Friday, March 29, 2013

PICHA MBALIMBALI ZIKIMUONESHA RAIS KIKWETE AONGOZA MAMIA KUUAGA MWILI WA MBUNGE WA CHAMBANI DAR ES SALAAM LEO


 Kaimu Katibu wa Bunge Mhe John Joel akisoma wasifu wa marehemu





 Rais jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Spika Anne Makinda alipowasili katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo Machi 29, 2013 kuongoza waombolezaji katika kuuaga mwili wa Mbunge wa Chambani(CUF),Salim Hemed Khamis aliyeanguka ghafla jana katika Vikao vya kamati ya Bunge na kufaikiri katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Baada ya shughuli hii mwili ulisafirishwa kuelekea Chambani, Pemba, kwa maziko.
 Rais jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Mbunge wa Monduli Mhe Edward Lowassa na Mbunge wa Mafia Mhe Abdulkarim Shah alipowasili katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo Machi 29, 2013 kuongoza waombolezaji katika kuuaga mwili wa Mbunge wa Chambani(CUF),Salim Hemed Khamis aliyeanguka ghafla jana katika Vikao vya kamati ya Bunge na kufaikiri katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Baada ya shughuli hii mwili ulisafirishwa kuelekea Chambani, Pemba, kwa maziko.
 Rais jakaya Mrisho Kikwete akitia saini kitabu cha maombolezo katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo Machi 29, 2013 na kuongoza waombolezaji katika kuuaga mwili wa Mbunge wa Chambani(CUF),Salim Hemed Khamis aliyeanguka ghafla jana katika Vikao vya kamati ya Bunge na kufaikiri katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Baada ya shughuli hii mwili ulisafirishwa kuelekea Chambani, Pemba, kwa maziko.
 Mama Salma Kikwete akitia saini kitabu cha maombolezo  katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo Machi 29, 2013 ambapo Rais Kikwete aliongoza waombolezaji katika kuuaga mwili wa Mbunge wa Chambani(CUF),Salim Hemed Khamis aliyeanguka ghafla jana katika Vikao vya kamati ya Bunge na kufaikiri katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Baada ya shughuli hii mwili ulisafirishwa kuelekea Chambani, Pemba, kwa maziko.
 Wabunge wanawake wakiwa katika maombolezo  katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo Machi 29, 2013 ambapo Rais Kikwete aliongoza waombolezaji  kuuaga mwili wa Mbunge wa Chambani(CUF),Salim Hemed Khamis aliyeanguka ghafla jana katika Vikao vya kamati ya Bunge na kufaikiri katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Baada ya shughuli hii mwili ulisafirishwa kuelekea Chambani, Pemba, kwa maziko.
 Rais jakaya Mrisho Kikwete akiwa na viongzi wa kitaifa na wabunge katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo Machi 29, 2013 ambako aliongoza waombolezaji katika kuuaga mwili wa Mbunge wa Chambani(CUF),Salim Hemed Khamis aliyeanguka ghafla jana katika Vikao vya kamati ya Bunge na kufaikiri katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Baada ya shughuli hii mwili ulisafirishwa kuelekea Chambani, Pemba, kwa maziko.

KOREA YA KASKAZINI YAELEKEZA MAKOMBORA MAREKANI NA KOREA YA KUSINI


Korea ya Kaskazini inasema imeyatega makombora yake ya kimkakati kuelekea Marekani na Korea ya Kusini.

http://si.wsj.net/public/resources/images/WO-AN202_KIM_G_20130328184120.jpgShirika la habari la Korea ya Kaskazini KCNA limemnukuu Rais Kim Jong Un akisema pindi pakitokea uchokozi kutoka Marekani,vikosi vya Korea ya Kaskazini vitalazimika kuishambulia Marekani pamoja na vituo vyake vya kijeshi vilivyoko katika visiwa vya bahari ya Pasifiki,Guam na Hawaii na vile vilivyoko Korea ya Kusini.Kim Jong Un ameamua hivyo kufuatia kutumwa na Marekani  madege mawili  chapa B-2 yenye uwezo wa kubeba makombora ya nuklea hadi Korea ya Kusini hapo jana.Waziri wa ulinzi wa Marekani Chuck Hagel amewaambia waandishi habari katika makao makuu ya wizara ya ulinzi-Pentagon- mjini Washington kwamba Marekani inazingatia kwa makini onyo lililotolewa na kwamba iko tayari kukabiliana na hali yoyote itakayojitokeza.

ULINZI WAIMARISHWA KIPINDI CHA PASAKA

POLISI imesema imeimarisha ulinzi kwenye maeneo yote ya kuabudia na maeneo mengine yenye mikusanyiko katika kipindi chote cha Sikukuu ya Pasaka, inayoanza kuadhimishwa leo kwa ibada ya Ijumaa Kuu.

http://api.ning.com/files/TdIQzJmQRty7mnDQTkaEpx2*gZfH6*A3BWKAB2kj23IE3p8KfjmezlnG-8gTkclBbMd8SZ6OXd5wt14iId0h6KyXzGpZRTVa/advera.jpg
Aidha, Polisi imewataka wananchi kuondoa hofu na kuwapuuza watu wachache, ama kikundi cha watu wanaotumia kipindi hiki cha sikukuu, kuwatia hofu kwa kusambaza ujumbe mfupi wa maneno wenye vitisho kwa watu mbalimbali kwa lengo la kuvuruga amani na utulivu.

Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Senso katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, alisema kitendo hicho cha kusambaza ujumbe ni uhalifu kama uhalifu mwingine na wakibainika hatua za kisheria, zitachukuliwa dhidi yao.

Senso alisema Polisi imejipanga kikamilifu kuimarisha usalama wa raia na mali zao kwa kipindi chote cha sikukuu, kwa kuwataka wananchi kusherehekea kwa amani na utulivu kuazia leo hadi Aprili mosi.

Alisema uzoefu unaonesha baadhi ya watu hutumia kipindi cha sikukuu, kufanya matukio ya uhalifu kutokana na mikusanyiko hiyo ya watu katika maeneo mbalimbali.

Wakati huo huo Polisi imewataka wamiliki wa kumbi za starehe, kuhakikisha usalama na kuzingatia uhalali na matumizi yake katika uingizaji wa watu kulingana na uwezo wake.

Wazazi pia wametakiwa kuwa makini na watoto hasa katika disko toto kuepuka ajali na matukio mengine yanayoweza kusababisha madhara juu yao. Wakati huo huo Ibada ya Ijumaa Kuu kitaifa, inafanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Usharika wa Dodoma Mjini.

Ofisa Habari wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Mchungaji John Kamoyo alisema kuwa Ibada hiyo itaongozwa na Askofu wa Dayosisi ya Dodoma, Amon Kinyunyu. Ibada ya Misa ya Sikukuu ya Pasaka, itafanyika Jumapili katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Paulo wa Msalaba mjini Dodoma.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Idara ya Mawasiliano wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Anatoly Salawa, ibada hiyo itaongozwa na Askofu wa Jimbo la Dodoma, Mhashamu Gervas Nyaisonga.

XI JINPING ATUA CONGO BRAZZAVILLE LEO


Rais Xi Jinping wa Jamhuri ya umma wa China amewasili leo Brazaville-mji mkuu wa Jamhuri ya Kongo-kituo cha mwisho cha ziara ya mataifa matatu barani Afrika.

MKUTANO WA WAANDISHI WA HABARI NA KAMISHINA WA POLISI ZANZIBAR


MAKAO  MAKUU YA POLISI ZANZIBAR
29.03.2013
Ndugu waandishi wa habari,
Assallam Aleykum
Najua leo ni siku ya mapumziko na siku ya ibada kwa waumini wote. Leo tupo katika Ijumaa Kuu lakini pia ni siku ya sala ya pamoja kwa Waislam katika misikiti mbalimbali. Nimeamua tukutane leo kwa sababu tatu. Kwanzza kwa kuendelea kudumisha doria za mjini na vijijini kwa kutumia gari, Askari wa migu, pikipiki na mbwa ili kuhakikisha usalama unadumu Visiwani hapa. Tunaendelea kutoa ushauri wa kiusalama na kushirikiana kwa karibu zaidi na wananchi wote kuona maisha na mali zao zinakuwa salama. Tunawaomba wenye mahoteli ya kitalii na nyumba za starehe kuwa karibuna jeshi lao la Polisi  pamoja na kufuata ushauri wote wa kiusalama wanaopewa kila wakati.
Pili tumeitana hapa kutoa shukurani kwa wananchi wote. Jeshi la Polisi linawashukuru wananchi wote kwa ujumla wao kwa ushirikiano mkubwa mnaotupa. Si rahisi kutaja kila msaada tunaopata kutoka makundi mbalimbali ya wananchi wteu, lakini tukiri msaada tunaopata ni mkubwa na umetusaidia na unaendelea kutusaidia katika kudumisha amani na utulivu. Hata hivyo, napenda kutoa shukurani zangu za dhanti kwa nyinyi waandhishi wa habari hasa wa ahapa Zanzibar kwa kuwa karibu na ofisi yang na kuchangia kwa kiwango kikubwa mchakato mzima wa kudumisha amani Visiwani hapa.
Jambo la tatu tuliloitania hapa ni kupeana taarifa juu ya maendelea ya kesi ya mauaji ya Padri Evarest Mushi. Najua si nyinyi tu waandishi wa habari lakini Watanzania wote wanatka kujua maendeleo ya upelelezi wa tukio hili. Jeshi la Polisi liliwaahidi litawajulisha kila hatua iliyofikiwa juu ya upelelezi wa shauri hili. Mpaka hapa tunapozungumza upelelezi wa shauri hili umefikia pahala pazuri na jalada la shauri hili limeshapalekwa kwa Mkurugenzi wa Mashitaka kwa hatua za kisheria. Muhusika wa mauaji haya tayari amekamatwa na ametambuliwa na watu walioshuhudia tukio hilo. Mtakumbuka Jeshi la Polisi mbali na hatua kadhaa za kiupelelezi walizozichukua ilikuwa ni pamoja na kuchora michoro ya sura ya mtu kwa kutumia  watu walioshuhudia tukio hilo. Baada ya kuitoa picha hiyo katika vyombo vya habari mablimbali vya kiulinzi, wananchi, vyombo vya habari na mitandao ya kijamii muhalifu hyo ametambulika na kutambuliwa.
Marehemu padre Evarist Mushi
Marehemu padre Evarist Mushi
Jeshi la Polisi liliahidi kutoa milioni kumi kwa watu watakaosaidia kupatikana kwa muhalifu huyo. Ahadi ile ipo pale pale na mwananchi aliyesaidia kutoa utambuzi Jeshi la Polisi litamzawadia kiwango hicho cha fedha, laini kwa usalama wa shahidi huyo na kwa sababu za kiupelelezi tukio la kumkabidhi fedha hizo hatutaliweka bayana katika vyombo vya habari.
Jeshi la Polisi linaendelea kuwaomba wananchi kutoa ushirikiano wa hali ya juu ili kufanikisha upelelezi wa matukio mengine yaliyopita. Tunawaahidi kuendelea kuwasisitiza na kutotoa siri wala kuwataja wale wote wanaotupa taarifa za kihalifu.
Mwisho kabisa, naomba niwashukuru tena wananchi wote wa Zanzibara kwa kuwa karibu na ofisi yangu na Jeshi la Polisi kwa ujumla katika mapambano ya vitendo vya kihalifu.
Ahsanteni.
Ijumaa karimu.
MUSSA A. MUSSA – CP
KAMISHNA WA POLISI
ZANZIBAR.

Thursday, March 28, 2013

WANARIADHA 300 WATHIBITISHA KUSHIRIKI MBIO ARUSHA APR 12


JUMLA ya wanariadha wapatao 300 wameshathibitisha kushiriki mbio za kumbukumbu za kifo cha hayati Waziri Mkuu na mpambanaji wa uhuru wa nchi hii, Edward Moringe Sokoine ambazo zinatarajiwa kufanyika Aprili 12 wilayani Monduli, Mkoani Arusha.


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgr5Y46BMjxH0pdKxaRbA1YUuWOFPE8wQWFqYOTO0m2sLV4zfA1cQtqCP7Mt3hhQ6PYZaoY8kcyOXOKH1QjhNZU4aQ5wGFDIHbHCo34LCnXVBaYbTMTWmeGb7Oz81wMWWgyXgH31oC-AAw/s1600/561482_419895221389529_204105510_n.jpg
Wanariadha kutoka katika mikoa ya, Kilimanjaro, Manyara, Tanga, Dar es salaam na Arusha wameshathibitisha kushirki katika mbio hizo za kwanza kufanyika katika historia ya nchi hii tangu uhuru.

Hayo yamebainishwa na mratibu wa mbio hizo ambaye pia ndiye mwongozaji wa mbio hizo, Wilhelm Gidabuday akizungumza,  kwa njia ya simu kutoka Dar es salaam na kusema kwamba tayari kupitia ofisi za chama cha Riadha mkoa Arusha (ARAA), wamethibitisha kushiriki mbio hizo.

Gidabuday alisema kuwa kujitokeza kwa wanariadha hao ni ishara nzuri kwani pamoja na kwamba ndio mara ya kwanza, kwa muitikio huo, wanatarajia kuwa na washiriki zaidi ya 500.

Kuhusu zoezi la usajili, Gidabuday alisema kuwa zoezi hilo litaanza mapema baada ya sikuukuu za Pasaka kumalizika na kuongeza kuwa zoezi hilo litafanyikia katika Ofisi za ARAA, zilizoko katika uwanja wa mpira wa miguu wa Sheikh amri Abeid jijini Arusha kwa ada ya sh. 2000 za Tanzania.

Sokoine Marathon inatarajia kukukutanisha watu wa kada mbalimbali, wakiwemo viongozi, wabunge, mawaziri na wananchi kwa ujumla kuadhimisha kumbukumbu ya kifo cha Hayati Waziri Mkuu wa Tanzania, Edward Moringe sokoine yatakayofanyika Aprili 12, wilayani Monduli katika kijiji alichozaliwa na kuzikwa.

Mbio hizo za umbali wa Kilomita 10 na kilomita 2 kutembea na kukimbia maandalizi yake kwa mujibu wa Waratibu wake mpaka sasa zimeshafikia hatua nzuri na kwa mujibu wa Waratibu wake, hatua zinazofanyika ni kufanya mazungumzo na Mgeni Rasmi ambaye kuna uwezekano akawa mmoja wa viongozi wakuu wa taifa hili.

Mwandishi: FADHIL ATHUMAN
Mhariri: JOHNSON JABIR

MMBUNGE SALIM HEMED KHAMIS KUPITIA TIKETI YA CUF - CHANBANI ZANZIBAR, AMEFARIKI DUNIA


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ITV Tanzania, imesema Mbunge kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF) aliyeanguka jana (Machi 27, 2013) katika mojawapo ya Kamati inayosimamiwa na Waziri Mkuu aliyejiuzulu Edward Lowassa, amefariki dunia baada ya kukimbizwa  hospitalini.

 

Mbunge wa Chambani Salim Hemed Khamis amefariki katika Hospitali ya Muhimbili alikokimbizwa jana na kupelekwa moja kwa moja katika Chumba cha Wagonjwa wanaohitaji uangalizi wa karibu(ICU).

CHANZO: ITV

WANAFUNZI 12 WAUAWA DAMASCUS - SYRIA


Mashambulio ya makombora katika chuo kikuu cha Damascus nchini Syria, yameua wanafunzi wasiopungua 12 leo. 

http://images.focus-news.net/85910b415b635384f3c76e9bf588d211.jpg
Televisheni ya nchi hiyo imewalaumu waasi ambao wamezidisha mashambulizi dhidi ya mji huo mkuu katika siku za hivi karibuni. Awali televisheni hiyo iliripoti kuwa watu kadhaa waliuawa au kujeruhiwa katika mashambulizi hilo dhidi ya kitivo cha usanifu cha Chuo Kikuu cha Damascus. Waasi wanaopambana kuuangusha utawala wa Assad wamezidisha mashambulizi ya makombora wiki hii dhidi ya maeneo ya kati mwa Damascus, ukiwemo uwanja wa Umayyad, yalipo makao makuu ya televisheni ya taifa. Shirika la uangalizi w ahaki za binaadamu nchini humo pia liliripoti mashambulizi hayo, lakini lilishusha idadi ya vifo kuwa 10.

MANDELA ALAZWA KWA MARADHI YA MAPAFU


Mandela alazwa tena hospitali

Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, amelazwa hospitali baada ya kupatwa tena na maambukizi katika mapafu yake. Hii ni mara ya pili ndani ya mwezi huu kwa mwanaharakati huyo, shujaa wa kupinga ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini, kulazwa hospitalini. 

Hapo Mwezi Disemba, Mandela alilazwa kwa wiki tatu hospitalini kwa maambukizi kama hayo na upasuaji wa kuondoka uvimbe tumboni. Mapema mwezi huu, Mandela alikaa hospitalini kwa usiku mmoja kwa ajili ya uchunguzi wa afya yake. 

Ofisi ya Rais Jacob Zuma imesema madaktari wanaendelea kumhudumia, kuhakikisha kuwa anapata matibabu bora zaidi ya kitaalamu na faraja. Mandela amekumbwa na maradhi kadhaa yanayotishia afya yake katika miaka ya hivi karibuni. 

Mapema mwaka 2012 alilazwa kwa ajili ya uchunguzi mdogo wa maumivu ya tumbo, na mwaka 2011 alilazwa kwa siku mbili kutokana na tatizo katika mfumo wa upumuaji.Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, amelazwa hospitali baada ya kupatwa tena na maambukizi katika mapafu yake. Hii ni mara ya pili ndani ya mwezi huu kwa mwanaharakati huyo, shujaa wa kupinga ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini, kulazwa hospitalini.

Hapo Mwezi Disemba, Mandela alilazwa kwa wiki tatu hospitalini kwa maambukizi kama hayo na upasuaji wa kuondoka uvimbe tumboni. Mapema mwezi huu, Mandela alikaa hospitalini kwa usiku mmoja kwa ajili ya uchunguzi wa afya yake.

Ofisi ya Rais Jacob Zuma imesema madaktari wanaendelea kumhudumia, kuhakikisha kuwa anapata matibabu bora zaidi ya kitaalamu na faraja. Mandela amekumbwa na maradhi kadhaa yanayotishia afya yake katika miaka ya hivi karibuni.

Mapema mwaka 2012 alilazwa kwa ajili ya uchunguzi mdogo wa maumivu ya tumbo, na mwaka 2011 alilazwa kwa siku mbili kutokana na tatizo katika mfumo wa upumuaji.

Wednesday, March 27, 2013

MWANAFUNZI UDSM AJINYONGA

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) mwaka wa pili Kitivo cha Sheria, Joseph Bernadina (25), amejinyonga kwa kutumia kamba na kukutwa ameifunga juu ya mti, katika eneo la Yombo chuoni hapo.

Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Utawala, Profesa Yunus Mgaya, alithibitisha  kutokea kwa tukio hilo na kwamba alipata taarifa hizo jana asubuhi.

Aliongeza kuwa Jumamosi iliyopita alipokea simu kutoka kituo cha polisi cha chuo hicho akielezwa kuwa kuna mwanafunzi alitishia kujiua, lakini aliwahishwa hospitali na kupatiwa ushauri kutoka kitengo maalum cha washauri wa chuoni hapo na kuruhusiwa Jumapili.

“Nilikuja tena kushtuka leo asubuhi napokea simu kutoka kwa mshauri wa wanafunzi kuwa kuna wanausalama wamemkuta mwanafunzi akiwa amejinyonga juu ya mti huku akiwa na karatasi kwenye mfuko wa sharti ikimtambulisha pamoja na ujumbe uliosema, kifo chake kisihusishwe na mtu yeyote kwani amejiua kwa ridhaa yake,” alisema.

Profesa Mgaya alisema taratibu za mazishi zinaendelea kufanywa na Uongozi wa chuo kwa kushirikiana na ndugu wa marehemu na kwamba Chuo kitagharamia kuusafirisha mwili kama alivyoomba katika ujumbe aliouacha wa kupelekwa wilayani Ludewa Mkoa wa Iringa.
Naye rafiki wa marehemu, Daniel Mwamlima, alisema marehemu hakuwahi kuzungumza chochote kilichoashiria kuwa ana matatizo wala mgogoro na mtu yeyote.

Alisema walimuacha hospitalini Jumamosi na kesho yake kumchukua, lakini  baadaye aliwatoroka. “Sasa leo (jana) asubuhi tulipata taarifa za mwanafunzi kujinyonga mbaya zaidi tukakuta ni yeye,” alisema Mwamlima. 

Waziri Mkuu wa Serikali ya Wanafunzi wa chuo hicho (Daruso), Yasini Athumani, alisema wamezipokea taarifa hizo kwa masikitiko makubwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, alithibitisha kutokea kwa tukio na alisema uchunguzi wa awali umebaini kwamba marehemu aliwahi kuwa na historia ya kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya kupata matibabu ya ugonjwa wa msongo wa mawazo.
CHANZO: NIPASHE

KOREA YA KASKAZINI YAKATA MAWASILIANO YA SIMU


Jeshi la Korea Kaskazini leo limekata mawasiliano ya simu na Korea Kusini, na kusitisha mawasiliano ya mwisho ya moja kwa moja baina ya nchi hizo mbili, katika wakati ambapo kuna hofu kubwa ya kijeshi.

 

http://msnbcmedia.msn.com/i/reuters/2013-01-01t024100z_1_cbre90007gg00_rtroptp_3_korea-north.jpgHatua hiyo imechukuliwa sambamba na tangazo kwamba viongozi wakuu wa kisiasa wa Korea Kaskazini watakutana katika siku chache zijazo kujadili kuhusu "suala muhimu" na kufanya uamuzi wa kurudi nyuma. Hatua ya kukata mawasiliano ya simu imetangazwa na afisa wa ngazi ya juu wa jeshi la Kaskazini kwa mwenzake wa kusini muda mfupi kabla ya kukatwa laini hizo za simu. Wiki chache zilizopita, Korea Kaskazini ilikata laini za simu za Shirika la Msalaba Mwekundu ambazo zilikuwa zimetumiwa katika mawasiliano ya kiserikali bila kuwepo uhusiano wa kidiplomasia. Hatua hiyo ya kukatwa mawasiliano ya simu ndiyo ya karibuni katika msururu wa vitisho na hatua kutoka serikali ya Pyongyang na kuongeza hofu katika Rasi ya Korea tangu uzinduzi wa Korea Kaskazini wa kombora la masafa marefu mwezi Desemba na majaribio yake ya nyuklia mwezi uliopita.

PICHA MBALIMBALI ZA JK AKIFUNGA MAFUNZO YA JKT KWA VIONGOZI HUKO HANDE-TANGA



Amiri Jeshi Mkuu,Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo ya muda mfupi kwa viongozi mbunge wa viti maalum Ester Bulaya leo katika kambi ya RUVU JKT.Rais Kikwete amefunga rasmi mafunzi hayo leo yaliyofanyika kwa wiki tatu.
Wabunge Halima Mdee na Ester Bulaya pamoja na wenzao wakila kiapo wakati wa kuhitimu mafunzo ya muda mfupi yaliyofanyika katika kambi ya jeshi la Kujenga Taifa Ruvu JKT huko kibaha Mkoani Pwani.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe, akipokea cheti cha kuhitimu mafunzo ya muda mfupi kwa viongozi kutoka kwa kaimu Mkuu wa
Mkoa wa Tanga, Muhingo Rweyemamu wakati wakimaliza mafunzo
ya JKT, katika Kambi ya Mgambo kikosi cha 835 wilayani Handeni Mkoa wa
Tanga. 
wakwanza katika mstari wa kushoto ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe anayefuata ni Mbunge wa Kinondoni Iddi Azani, wakiwa kwenye Paredi ya kumaliza mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT Kikosi cha
835 Mgambo JKT kambi iliyopo katika Kata ya Mgambo ilayani Handeni Mkoa wa Tanga.
wakwanza kushoto ni Mbunge wa Kinondoni Iddi Azani pamoja na Mbunge
wa Kigoma Kaskazini, ZItto Kabwe, wakihitimu mafunzo ya JKT katika kambi ya 835 Mgambo JKT iliyopo Tarafa ya Mzundu wilayani Handeni Mkoa wa Tanga.
Mbunge wa Kinondoni Iddi Azani, akiapa wakati wa kumaliza mafunzo ya
JKT katika Kambi ya 835 ya Mgambo JKT, iliyopo katika Tarafa ya Mzundu
wilayani Handeni Mkoa wa Tanga.
Mbunge wa Biharamulo, Dk Athanas Mbassa, akiapa wakati wa kumaliza
mafunzo ya JKT katika Kambi ya 835 ya Mgambo JKT, iliyopo katika Tarafa ya Mzundu wilayani Handeni Mkoa wa Tanga. 
Mbunge wa Kiwani Pemba, Abdallah Haji Ali, , akiapa wakati wa
kumaliza mafunzo ya JKT katika Kambi ya 835 ya Mgambo JKT, iliyopo katika Tarafa ya Mzundu wilayani Handeni Mkoa wa Tanga.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe, akiapa mbele ya kaimu Mkuu wa
Mkoa wa Tanga, Muhingo Rweyemamu, hayupo pichani, wakati wakimaliza mafunzo ya JKT, katika Kambi ya Mgambo kikosi cha 835 wilayani Handeni Mkoa wa Tanga.
Mbunge Viti maalum Raya Khamis , akiapa wakati wa kumaliza mafunzo ya
JKT katika Kambi ya 835 ya Mgambo JKT, iliyopo katika Tarafa ya Mzundu
wilayani Handeni.
Baadhi ya Wabunge walikuwa wakichukua mafunzo ya muda mfupi kwa viongozi katika Kambi ya Mgambo kikosi cha 835 wilayani Handeni Mkoa wa Tanga.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na waheshimiwa wabunge waliohitimu mafunzo maalumu ya JKT.
Mbunge wa Mtera Mh. Livingstone Lusinde  Kibajaji"  (wa tatu toka kulia) akipiga kwata leo huko Ruvu.




Picha Zote za Tanga na Hussein Semdoe.

TIANGAYE YU BADO YU MADARAKANI

Waziri Mkuu katika utawala ulioangushwa wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Nicolas Tiangaye amesema amechaguliwa tena katika wadhifa huo wakati watawala wapya wa mapinduzi wakijaribu kurejesha utulivu na kutafuta imani ya jamii ya kimataifa. 
http://www.rfi.fr/sites/filesrfi/imagecache/rfi_43_large/sites/images.rfi.fr/files/aef_image/000_Par7433883_0.jpgMamlaka yamerudi tena mjini Bangui, siku nne baada ya Michel Djotodia na kundi lake la waasiw a SELEKA kuutwa mji huo mkuu, hali iliyomlazimu rais Francois Bozize kutoroka. Bozize ambaye alitwaa madaraka katika mapinduzi ya mwaka wa 2003, ameonekana nchini Cameroon, ambako maafisa wanasema anasubiri kusafirishwa hadi nchi nyingine. Nicolas Tiangaye, ambaye ni wakili na mtetezi wa haki za binaadamu, alipewa wadhifa wa waziri mkuu kufuatia makubaliano ya Januari chini ya mkataba wa kugawana mamlaka baina ya Bozize na waasi wa SELEKA, na ambao ulimaliza uasi wa kwanza. Kiongozi wa mapinduzi Djotodia amevunja bunge na kutangaza kuwa ataongoza kwa kuzingatia mkataba huo wa Januari uliotiwa saini mjini Libreville, Gabon.

Monday, March 25, 2013

KAJALA AHUKUMIWA MIAKA 5 AU FAINI MIL 13, WEMA AJIANDAA KUMLIPIA


HUKUMU ya kesi iliyokuwa inamkabili staa wa filamu za Kibongo, Kajala Masanja na mumewe imetolewa leo na Hakimu Sundi Fimbo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar. Katika hukumu hiyo Kajala amehukumiwa kwenda jela miaka mitano au kulipa faini ya shilingi milioni 13 na mumewe kwenda jela miaka mitano au kulipa faini ya shilingi milioni 213.
Msanii Kajala Masanja pamoja na Wema.
Kajala alikuwa anakabiliwa na kesi ya kuuza nyumba iliyowekwa kizuizini na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) baada ya mumewe, Faraji Agustino kukumbwa na msala wa kutakatisha fedha haramu.
Taarifa tulizozipata ni kwamba msanii Wema Sepetu anajiandaa kupeleka faini ya shilingi milioni 13 ili kumnusuru na kifungo msanii mwenzake.
Taarifa zaidi tutazidi kuwajulisha.



TENGA AWAPONGEZA WACHEZAJI WA TAIFA STARS

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga amewapongeza wachezaji wa Taifa Stars na benchi lao la ufundi, washabiki, mdhamini na Serikali kwa kufanikisha ushindi wa jana.

http://2.bp.blogspot.com/-PPp2IXpaP5Y/Txk52BJmw9I/AAAAAAAAETQ/DDznTiZJz4Y/s400/tff+LOGO.jpg
Tenga amesema ushindi huo umetokana na ushirikiano kutoka kwa wadau wote, na hasa wachezaji walioonesha kiwango kikubwa kulinganisha na mechi zilizopita ikiwemo kiwango cha kujituma uwanjani.

Amesema Serikali ni mdau mkubwa wa mpira wa miguu katika miundombinu, usalama na idara zake mbalimbali ikiwemo Uhamiaji ambayo imefanikisha kwa kiasi kikubwa kuwepo kwa mechi hiyo ambapo Taifa Stars iliifunga Morocco mabao 3-1.

CHADEMA YAKUBALI KUSITISHA MAANDAMANO


HATIMAYE Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimekubali kusitisha maandamano yake yaliyokuwa yafanyike leo katika majiji manne ya Dar es Salaam, Arusha, Mbeya na Mwanza, kuwashinikiza Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa na Naibu wake, Philipo Mulugo kuachia ngazi.

http://blog.tanzaniamwandi.co.tz/wp-content/uploads/2012/06/chadema.png?width=338
Hatua hiyo imefikiwa baada ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Said Mwema akiwa pamoja na Kamishina wa Oparesheni (CP) Paul Chagonja, Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleimani Kova na maofisa wengine kukutana na viongozi wa CHADEMA chini ya Mwenyekiti, Freeman Mbowe.

CHADEMA iliwapa viongozi hao wiki mbili tangu Februari 18 mwaka huu, kuachia ngazi kama sehemu ya uwajibikaji kutokana na matokeo mabaya vinginevyo wangefanya maandamano makubwa leo kuwashinikiza wang’oke.

Hata hivyo, juzi serikali ilitangaza kuyasitisha maandamano hayo ikidai inatoa nafasi kwa wananchi waweze kumpokea Rais wa China, Xi Jinping ambaye alianza ziara ya siku mbili nchini, jambo ambalo CHADEMA walilipinga na kusisitiza kuandamana.

Jana viongozi hao wa polisi na siasa walilazimika kukutana na kuzungumza kwa kirefu na Mbowe hatimaye kufikia muafaka kwa CHADEMA kukubali kusogeza maandamano yao hadi hapo baadaye.

WAWILI KORTINI KWA KUKUTWA NA BANGHI YENYE THAMANI YA TZS MILIONI 197


Watu wawili wakazi wa Kijiji cha Kitendeni Wilayani Siha mkoani Kilimanjaro wameshikishwa katika mahakama ya Hakimu mkazi ya Wilaya ya Hai kwa kosa la kupatikana na madawa ya kulevya aina bangi  kilo 197  yenye thamani ya  shilingi  milioni  97.

MAREKANI YAKABIDHI GEREZA LA BAGRAM KWA KARZAI


Marekani imeikabidhi Afghanistan udhibiti kamili wa gereza la Bagram, hatua ambayo imeondoa kizingiti kikubwa katika uhusiano baina ya nchi hizo mbili, wakati majeshi ya kimataifa yanayoongozwa na Marekani yakijiandaa kuondoka nchini Afghanistan, baada ya vita vya zaidi ya muongo mmoja. 

MAHAKA YA JUU KENYA YATAKA KUHESABIWA KURA UPYA VITUO 22


Mahakama ya Juu nchini Kenya imeamuru kura zihesabiwe upya katika vituo 22, kufuatia uchaguzi wa urais ambao uliepuka duru ya pili kwa kura chache.

JAMBAZI MAARUFU LAUAWA MBEYA


MTU mmoja ambaye anasadikiwa kuwa ni jambazi ameuawa kwa kupigwa risasi na Askari wa Jeshi la Polisi akiwa kwenye harakati za kuteka magari katika Eneo la Mlima Nyoka Jijini Mbeya baada ya kutokea kwa majibizano ya kurushiana risasi.

  
ACP DIWANI ATHUMANI NA JAMBAZI MOCHWARI RUFAA MBEYA
Jambazi huyo ni miongoni mwa watu waliokuwa wakitafutwa na Jeshi la Polisi Mkoani hapa akituhumiwa kuhusika na mauaji ya Askari Polisi mwenye namba G 68 PC Jafari yaliyotokea  Februari 6, Mwaka huu  katika eneo la Matundasi Wilayani Chunya.
  
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani amethibitisha kutokea kwa tukio hilo katika Mkutano alioufanya na waandishi wa Habari Ofisini kwake ambapo amesema tukio hilo limetokea   majira ya Saa 10(kumi) Alfajiri usiku wa kuamkia leo Machi 25, Mwaka huu.
  
Kamanda Diwani amesema kabla ya tukio majambazi wapatao wanne  tayari walikuwa wameweka mawe barabarani kwa nia ya kuteka magari ili wafanye uporaji katika eneo hilo la Mlima Nyoka ambalo limekuwa na matukio kadhaa ya watu kuporwa mali zao.
  
Amesema Jeshi la polisi baada ya kupata habari za kutegwa mawe, askari walifika kwa wakati kwa kuwa polisi walikuwa jirani na eneo hilo na kuweka mtego kwa kuwa majambazi hawakuwa wameonekana kwa wakati ule.
  
Diwani alisema katika mapambano hayo alijeruhiwa jambazi mmoja kwa risasi kiunoni na ubavuni kulia na wengine watatu walifanikiwa kutoroka ambapo Marehemu alipowahishwa hospitali kwa matibabu daktari alibaini kuwa amekwisha fariki.
  
Amesema  jambazi huyo alikutwa na silaha moja SMG yenye namba  AB huku namba  nyingine zikiwa zimefutwa na magazine yake ikiwa na risasi ishirini na mbili (22) pamoja na mapanga mawili(2).
  
Baada ya  Marehemu kufanyiwa upekuzi maungoni mwake jambazi huyo alikutwa na kitambulisho cha mkazi chenye namba B.0010453 chenye jina la Emanuel Blasius Mdendemi aliyezaliwa mwaka 1984 eneo la Matamba wilayani Makete Mkoa wa Iringa makazi yake ni Uwemba Mkoani Njombe.
CHANZO: MBEYA YETU

Sunday, March 24, 2013

TAIFA STARS YA TANZANIA YAIFUNGA LIONS OF THE ATLAS YA MOROCCO


Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wamewainua watanzania kwa kumzaba Morocco mabao 3-1 katika mechi ya kuwania kufuzu kucheza Kombe la Dunia.

POLISI ALIYEAUA NAYE AUAWA

ASKARI Polisi PC Yohana mwenye namba 7771 amemuua kwa kumpiga risasi mwendesha bodaboda, Makisio Ngonyani (27), kisha naye akauawa na watu wenye hasira kwa kutumia mawe na mbao.

PICHA MBALIMBALI ZA KILIMANJARO VAISAKHI RALLY SECTION YA ISMAIL-SANYA CHINI

Mashindano ya Magari mwaka huu maarufu kwa jina la Kilimanjaro Vaisakhi Rally yanaendelea katika wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro.



Katika kituo cha Ismail Sanya Chini ikiwa ni miongoni mwa Section za kupita magari ya mbio msimu huu mambo yalikuwa kama hivi katika picha mbalimbali:-
 








MTOTO AFA KWA KUTUMBUKIA KISIMANI


MTOTO Kalebi Martine mwenye mwaka mmoja, amefariki dunia muda mfupi baada ya kutumbukia katika kisima chenye urefu wa mita tatu kilichopo jirani na nyumba aliyokuwa anaishi.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minagi alisema tukio hilo lilitokea juzi jioni maeneo ya Tabata-Kimanga ambapo mtoto huyo alikuwa anacheza na wenzake kwa jirani yake aitwaye Bilali Ally (43).

Minagi alisema kuwa kwa mujibu wa mtoa taarifa Martine Alexandria (33) ambaye ni baba mzazi wa mtoto huyo, baada ya mtoto wake kutumbukia aliokolewa na watu waliokuwepo katika eneo hilo.

Alisema mtoto huyo alifariki dunia wakati akiwa njiani kumpeleka hospitali na mwili wake umehifadhiwa katika hospitali ya Amana kwa upelelezi zaidi.

Katika tukio lingine, mkazi wa Bunju, Patrick Chuwa (28) amefariki dunia papo hapo baada ya kusukumwa barabarani na kukanyagwa na gari.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni Charles Kenyela alisema tukio hilo lilitokea juzi asubuhi maeneo ya barabara ya Sam Nujoma, Mwenge ambapo Chuwa alikuwa akivuka barabara kutoka kushoto kwenda kulia.

Kenyela alisema kuwa ajali hiyo ilitokea baada ya gari aina ya Toyota Land Cruiser yenye namba za usajili T 126 AXK iliyokuwa ikiendeshwa na Zakiel Mwangike (52) mkazi wa Mbezi Beach akitokea Ubungo kumsukuma Chuwa na kuanguka barabarani.

Alisema Chuwa akiwa bado chini barabarani, alikanyagwa kichwani na gari aina ya DAF yenye namba za usajili T 635 CEK iliyokuwa ikiendeshwa na Selestina Segwa (45) na kusababisha kifo chake papo hapo.

Kamanda huyo alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Mwananyala na madereva wa magari yote mawili wameshikiliwa na polisi kwa upelelezi zaidi.

CHANZO: TANZANIA DAIMA