Saturday, February 9, 2013

HAWA NDIO BINADAM WALIVYO

1. Wakikukwepa usijali. Ipo siku watakutafuta.
2. Wakikusengenya nyamaza. Huenda watanyamaza.
3. Wakikununia omba Mungu. Ipo siku Watakuchekea.
4. Wakikupongeza uswaamini saana. Labla wanakukashifu!
5. Wakikutenga achana nao kwakua hawana MBINGU ya kukuweka na wao sio kila kitu.
6. Wakikudhulumu. Shukuru Mungu atakulipa marambili zaidi.
7. Wakikualika kuamakini. Isiwe wanakutega tuu.
HATA YESU ALIPENDWA HIVYO MPAKA AKASULUBIWA MSALABANI NA SASA YU HAI AMEFUFUKA.

Friday, February 8, 2013

Tanzia: Askofu Mstaafu Amedeus Msarikie wa Moshi, Afariki Dunia


Askofu Mstaafu Amedeus Msarikie
Askofu mstaafu Amedeus Msarikie wa Jimbo Katoliki Moshi, Tanzania amefariki dunia Alhamisi, tarehe 7 Februari 2013 mjini Nairobi, Kenya alikokuwa akitibiwa saratani ya kibofu cha mkojo.

Kwa mujibu wa Radio Vatikani, habari za msiba zimethibitishwa na Askofu Isack Amani wa Jimbo Katoliki Moshi. Mipango ya maziko inaandaliwa na Jimbo, pia mazishi yatafanyika tarehe 14 February 2013.

Askofu Msarikie alizaliwa Kirua Vunjo Moshi, mwaka 1931. Alipewa daraja la Upadre tarehe 8 Agosti 1961 kama padre wa Jimbo la Moshi. Aliteuliwa na Baba Mtakatifu Yohani Paulo II kuwa askofu wa Jimbo la Moshi tarehere 21 Machi 1986. Alisimikwa rasmi kama askofu wa Jimbo la Moshi tarehe 1 Mei 1986 na Askofu Jozef Kadinali Tomko akisaidiwa na Makadinali Laurian Rugambwa na Maurice Michael Otunga.

Baada ya kulitumikia Kanisa la Moshi kwa miaka 26, Askofu Amedeus alistaafu kwa mujibu wa sheria ya Kanisa tarehe 21 Novemba 2007. Baada ya kustaafu, aliendelea kulihudumia kanisa kwa huduma mbali mbali za kiroho na kimwili. Jimbo la Moshi kwa sasa linaongozwa na Mh. Askofu Isaac Amani Massawe tangu Novemba 2007.

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU
MAHALI PEMA PEPONI
AMINA