Mkuu wa wilaya ya Singida
mwalimu Queen Mlozi (wa pili kushoto) akikagua ujenzi wa maabara tatu za
shule ya sekondari kata ya Mitunduruni jimbo la Singida mjini.Wa
kwanza kushoto ni diwani wa kata ya Mitunduruni,Sorongai Pantaleo.
Diwani wa kata ya Mitundurinu
(CCM) jimbo la Singida mjini,Sorongai Pantaleo (wa kwanza kushoto)
akizungumza na mkuu wa wilaya ya Singida mwalimu Queen Mlozi ofisini kwa
mkuu wa shule ya sekondari kata ya Mitunduruni.
Mkuu
wa wilaya ya Singida,mwalimu Queen Mlozi, (wa pili kutoka kulia)
akikagua ujenzi wa choo katika shule ya msingi ya Unkyankindi kata ya
Mitunduruni.Wa kwanza kulia ni diwani wa kata ya Mitunduruni Bw.Sorongai
Pantaleo.
Baadhi ya vyumba vya madarasa vilivyojengwa na mbunge wa jimbo la Singida mjini,Mohammed Gullam Dewji.
Mkuu
wa wilaya ya Singida Mwalimu Queen Mlozi amewahimiza wakuu wa shule za
sekondari kuwa wabunifu katika kutafuta misaada na fedha kwa ajili ya
kugharamia ujenzi wa maabara.
Amesema
kwa vile sio rahisi kwa serikali kufanya kila kitu ikiwemo kujenga kwa
mpigo maabara katika shule zote za sekondari nchini, kuna umuhimu mkubwa
kwa wananchi na wadau wengine kusaidiana na serikali.
Mkuu
huyo wa wilaya ametoa changamoto hiyo wakati akizungumza na