Marekani imeikabidhi Afghanistan udhibiti kamili wa gereza la Bagram, hatua ambayo imeondoa kizingiti kikubwa katika uhusiano baina ya nchi hizo mbili, wakati majeshi ya kimataifa yanayoongozwa na Marekani yakijiandaa kuondoka nchini Afghanistan, baada ya vita vya zaidi ya muongo mmoja.
Kamanda wa vikosi vya kimataifa nchini Afghanistan, Jenerali Joseph Dunford, amesema katika taarifa yake kwamba makabidhiano hayo yanaonyesha kuimarika na kujiamini kwa Afghanistan. Bagram lilikuwa gereza pekee chini ya udhibiti wa Marekani nchini Afghanistan, na serikali za nchi mbili zilikubaliana mwaka mmoja uliopita kuwa lingekabidhiwa kwa Afghanistan.
Rais Hamid Karzai wa Afghanistan alikuwa amekuita kukabidhiwa gereza hilo kama hatua muhimu ya kurejesha uhuru wa nchi yake juu ya masuala muhimu kutoka kwa Marekani. Marekani kwa upande wake ilikuwa na wasiwasi kwamba kulikabidhi gereza hilo lenye wafungwa wa Taliban na Al-Qaida kwa serikali dhaifu ya Afghanistan, kungewapa fursa wafungwa hao kurudi kwenye uwanja wa vita.
No comments:
Post a Comment