Friday, March 29, 2013

KOREA YA KASKAZINI YAELEKEZA MAKOMBORA MAREKANI NA KOREA YA KUSINI


Korea ya Kaskazini inasema imeyatega makombora yake ya kimkakati kuelekea Marekani na Korea ya Kusini.

http://si.wsj.net/public/resources/images/WO-AN202_KIM_G_20130328184120.jpgShirika la habari la Korea ya Kaskazini KCNA limemnukuu Rais Kim Jong Un akisema pindi pakitokea uchokozi kutoka Marekani,vikosi vya Korea ya Kaskazini vitalazimika kuishambulia Marekani pamoja na vituo vyake vya kijeshi vilivyoko katika visiwa vya bahari ya Pasifiki,Guam na Hawaii na vile vilivyoko Korea ya Kusini.Kim Jong Un ameamua hivyo kufuatia kutumwa na Marekani  madege mawili  chapa B-2 yenye uwezo wa kubeba makombora ya nuklea hadi Korea ya Kusini hapo jana.Waziri wa ulinzi wa Marekani Chuck Hagel amewaambia waandishi habari katika makao makuu ya wizara ya ulinzi-Pentagon- mjini Washington kwamba Marekani inazingatia kwa makini onyo lililotolewa na kwamba iko tayari kukabiliana na hali yoyote itakayojitokeza.

No comments:

Post a Comment