Mashambulio ya makombora katika chuo kikuu cha Damascus nchini Syria, yameua wanafunzi wasiopungua 12 leo.
Televisheni ya nchi hiyo imewalaumu waasi ambao wamezidisha mashambulizi dhidi ya mji huo mkuu katika siku za hivi karibuni. Awali televisheni hiyo iliripoti kuwa watu kadhaa waliuawa au kujeruhiwa katika mashambulizi hilo dhidi ya kitivo cha usanifu cha Chuo Kikuu cha Damascus. Waasi wanaopambana kuuangusha utawala wa Assad wamezidisha mashambulizi ya makombora wiki hii dhidi ya maeneo ya kati mwa Damascus, ukiwemo uwanja wa Umayyad, yalipo makao makuu ya televisheni ya taifa. Shirika la uangalizi w ahaki za binaadamu nchini humo pia liliripoti mashambulizi hayo, lakini lilishusha idadi ya vifo kuwa 10.
No comments:
Post a Comment