Watu wawili wakazi wa Kijiji cha Kitendeni Wilayani Siha mkoani Kilimanjaro wameshikishwa katika mahakama ya Hakimu mkazi ya Wilaya ya Hai kwa kosa la kupatikana na madawa ya kulevya aina bangi kilo 197 yenye thamani ya shilingi milioni 97.
Akisoma hati ya mashitaka mahakani hapo mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa Wilaya ya Hai, Denis Mpelembwa, Mwendesha mashitaka wa polisi wa Wilaya ya Siha Roymax Membe alisema watu hao walipatikana na madawa hayo ya kulevya kinyume na kifungu cha sheria namba 12(d)cha udhibiti wa madawa kulevya sura 95 ya mwaka 2002
Membe amewataja watu hao kuwa ni Samweli Melekzedeck (33) na Melta Kuya ambapo alisema kuwa watu hao walipatika na madawa hayo mnamo Machi 18 mwaka majira ya saa 3 asubuhi katika kijiji cha Kitendeni katika mazingira ambayo yaliashiria madawa hayo yalikuwa kwa ajili ya biashara
Mwendesha mashitaka huyo aliiomba mahakama kutowapatia dhamana watuhumiwa hao kutokana na kiasi cha madawa hayo kuwa ya thamani kubwa kwani alisema kwa mujibu wa sheria ya menendo wa kesi za jinai mtuhumiwa anapokuwa ametenda kosa lenye kiasi cha fedha zaidi ya shilingi milioni kumi hastahili dhamana.
Alifafanua kuwa pamoja na watuhumiwa hao kufikishwa mahakamani hapo upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na kuiomba mahakama hiyo kutaja tarehe nyingine ya kusikiliza kwa kesi hiyo
Hata hivyo watuhumiwa wote walikana na shitaka na Hakimu anayeskiliza kesi hiyo alikubaliana na ombi la mwendesha mashtaka wa polisi na kuharisha kesi hiyo hadi Aprili 4 mwaka huu itakapo tajwa tena na watuhumiwa wapo rumande
No comments:
Post a Comment