Tuesday, April 16, 2013

LAIZER AWATAKA WAFUGAJI WA KIMASAI KUPUNGUZA MIFUGO KWA KUUZA

Mbunge wa Jimbo la Longido Michael Lekule Laizer kwa titketi ya Chama cha Mapinduzi amewataka wafugaji wa kimasai katika Jimbo lake kupunguza mifugo hiyo kwa kuiuza ili kuongeza mapato yatokanayo na mifugo yao.

Katika mahojiano mapema leo asubuhi Mheshimiwa Lekule Laizer amesema endapo wafugaji wa kimasai watatambua kuwa mifugo waliyonayo ni rasimali tosha ya wao kukua kiuchumi basi itasaidia jimbo lake kuwa katika hali nzuri.

Laizer amesema kwa muda mrefu sasa kauli mbiu ya kupunguza mifugo imeonekana kutozaa matunda kutokana na mila na desturi za kimasai kutotaka kupunguza mifugo hiyo.

Pia ameongeza kusema kwa sasa kuna mabadiliko ya tabia nchi ambapo yamefanya hata mifugo kutoweza kufugika kwani hata katika jimbo lale kulitokea maafa ya ng’ombe kufa kutokana na misimu mitatu ya mvua kutonyesha katika ardhi yao.

Laizer amesema endapo watauza mifugo hiyo watatakiwa kuweka fedha zao benki kwa ajili ya matumizi mbalimbali ikwemo kujenga nyumba, kusomesha watoto.

Aidha Mbunge huyo amesema tangu mwaka 1995 alipoingia madaraka kulisimamia jimbo hilo amewatendea wananchi mahitaji muhimu huku akitajihidi kupitia serikali ya CCM iliyopo madaraka kukamilisha ahadi zake kwa wananchi.

BOSTON MARATHON ZA SABABISHA VIFO MAREKANI


Mpaka sasa watu watatu wameshakufa kutokana na mashambulio ya mabomu mawili yaliyoripuka wakati wa mbio ndefu za marathon katika mji wa Boston nchini Marekani. 

Mashambulio ya mabomu, BostonMabomu mawili yaliripuka kwenye mitaa iliyokuwa imejaa watu karibu na sehemu ya kumalizia mbio za marathon. Watu wasiopungua watatu wamekufa kutokana na miripuko ya mabomu hayo yaliyoutikisa mji wa Boston katika jimbo la Marekani la Massachusettes.

Je ni magaidi tena?
Watu wengine zaidi ya140 walijeruhiwa katika kadhia ya umwagikaji wa damu. Vioo vilivunjika na sehemu za miili ya binadamu ilitapakaa- hali iliyosababisha wasiwasi kwamba magaidi wameishambulia tena Marekani. Msemaji wa Ikulu ya Marekani ambae hakutaka kutajwa kwa sababu uchunguzi bado unaendelea, ameeleza kuwa mashambulio hayo yanazingatiwa kuwa ni kazi ya magaidi.

Akitoa tamko juu ya mashambulio hayo Rais Obama aliepuka kutumia neno gaidi, alieleza kwamba maafisa wa Marekani hawajui ni nani aliyeyatega mabomu hayo na kwa nini. Hata hivyo afisa mmoja wa Ikulu ya Marekani alisema baadae kuwa miripuko hiyo iliyotokea kwenye mbio za marathoni zenye jadi ya miaka mingi, inazingatiwa kuwa kitendo cha ugaidi.

Obama asema aliefanya mashambulio atapatikana:
Rais Obama alilihutubia taifa kwa kuwahakikishia Wamarekani kwamba, tukio hilo litachunguzwa kwa undani. Obama alisema "Tutabainisha nani ameyafanya mashambulio haya na kwa sababu gani." Ameeleza kuwa wote wale waliohusika, au kikundi chochote- kitauona mkono mkali wa sheria. Rais Obama amesema Marekani itamjua alieyafanya mashambulio hayo.

Mabomu hayo mawili yalipishana kwa muda wa sekunde chache tu. Mwokoaji anaetoa huduma ya kwanza, amesema wanajaribu kupata damu kwa haraka. Amearifu kuwa wapo waliojeruhiwa kwa kukatika viungo vya mwili na, wengine waliumizwa na vipande vya vioo, na pote palisambaa damu.

CHANZO: DW/DPA