VITA dhidi ya biashara ya madawa ya kulevya ni ngumu sana, dirisha la
mafanikio ya kudhibiti linafungwa na vigogo wauza unga ambao wana fedha
nyingi zinazoyumbisha sheria kuchukua mkondo wake.
Pointi nambari moja ni uwepo wa ripoti za ukamatwaji wauza unga
lakini hukumu hazitolewi, swali kwa nini hawahukumiwi likipashwa moto
ili kuunguza mamlaka zinazohusika, linafichua siri nzito kuhusu
madai ya vigogo waliokamatwa na kuachiwa.
Watu wanne ambao wanatajwa kuwa miongoni mwa vinara wa madawa ya
kulevya nchini, walikamatwa na madawa ya kulevya yenye thamani ya
shilingi bilioni 6.2 kisha wakafikishwa mahakamani ambako inadaiwa
wameachiwa katika mazingira tatanishi.
Abdul.
Vigogo hao wanne, wapo Watanzania wawili na wengine ni raia wa
Pakistan ambao sasa hivi inadaiwa wameshatoroka kwenda nje ya nchi.MCHEZO ULIKUWAJE?
Februari 21, 2011, jeshi la polisi kupitia kitengo cha kudhibiti na kupambana na madawa ya kulevya, kiliwakamata wafanyabiashara hao ambao majina yao ni William Chonde na Kambi Zuberi (Watanzania) pamoja na Wapakistan, Abdul Ghan Peer Bux na Shahbaz Malk.
Kambi.
Watu hao, walikamatwa na mzigo huo Mbezi Jogoo, Dar es Salaam kwenye
nyumba ya Chonde, wakiwa na madawa ya kulevya aina ya heroine, yenye
uzito wa kilo 179 ambayo thamani yake ni shilingi 6,265,000,000.
Sera ya ni kuendeleza safari iliyoianzisha kwa vile ndilo
liliandika pale walipokamatwa zaidi ya miaka miwili iliyopita. Wiki
mbili zilizopita, lilianza upekuzi kujua kesi hiyo imefikia wapi.
Uchunguzi wa waandishi wetu uliweza kubaini kuwa watuhumiwa hao wa
madawa ya kulevya waliachiwa na mahakama kuu kwa dhamana, kinyume na
sheria ya madawa ya kulevya inavyoeleza.
Shahbaz.
SHERIA INASEMAJE?
Sheria ya madawa ya kulevya ya mwaka 1996, sura
ya 95, kipengele nambari 9, kifungu nambari 27, kifungu kidogo nambari
1A, kinasema: “Yeyote atakayekamatwa na madawa ya kulevya yenye thamani
zaidi ya shilingi milioni 10 hapaswi kupewa dhamana.”
Vilevile,
sheria hiyo inaendelea katika kifungu kidogo nambari 1B ambacho
kinasema: “Yeyote atakayekamatwa akisafirisha madawa ya kulevya hapaswi
kudhaminiwa.”
Fred.
KAMANDA MADAWA YA KULEVYA ALIA
Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti na
Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa, alipoulizwa
kuhusu kile anachokifahamu kufuatia kuachiwa kwa watuhumiwa hao,
alijibu:
“Mimi sijui, waliachiwa mahakamani. Kazi yetu sisi ilikuwa
ni kuwakamata, kila kitu kikapelekwa kwa DPP (mkurugenzi wa mashtaka),
baada ya hapo kesi ilikwenda kwa msajili wa mahakama.
“Nijuavyo mimi ni kwamba walifikishwa mahakamani na nilisikia waliachiwa kwa dhamana,” alisema Nzowa.
Kamanda Nzowa.
KWA NINI WATUHUMIWA WALIACHIWA NA KUPEWA HATI ZA KUSAFIRIA?
Yapo
madai kwamba baada ya watuhumiwa hao kupewa dhamana, walikabidhiwa hati
za kusafiria (passport) ambazo ziliwawezesha kutoroka.;
UWAZI: Unaweza kufahamu kigezo kipi kilitumika kuwapa dhamana watuhumiwa hao? Maana sheria inakataza.
NZOWA: Nadhani mahakama ndiyo inapaswa kuulizwa swali hilo. Siwezi kuisemea, maana ule ni mhimili mwingine huru.
UWAZI: Inadaiwa wewe ndiye uliwapa passport zao na sasa tunaambiwa walishatoroka nchini, hili limekaaje?
NZOWA: Ni kweli tuliwapa passport zao, tuliagizwa na mahakama kufanya hivyo.
MSAJILI WA MAHAKAMA KUU
Msajili wa Mahakama Kuu, Benedict
Mwingwa, alipoulizwa kuhusu kuachiwa kwa watuhumiwa hao kwa dhamana,
aling’aka, kisha akaahidi kufuatilia kujua kisa na mkasa.
“Nimeshtushwa sana na hilo jambo. Ni kweli sheria inakataza, sasa
watuhumiwa kama hao hawakupaswa kudhaminiwa. Nalifanyia kazi, nitakutana
na jaji anayesikiliza kesi hiyo aniambie sheria aliyotumia,” alisema
Mwingwa.
MOTO UNAWAKA
Uchunguzi wa Uwazi umebaini kwamba baada ya
malalamiko ya muda mrefu kuhusu kusuasua kwa kesi za madawa ya kulevya
ambayo yanaelekezwa Mahakama Kuu, Jaji Kiongozi, Fakhi Jundu, aliitisha
mkutano wa dharura wiki mbili zilizopita.
Mkutano huo ulishirikisha
majaji wa mahakama kuu, idara ya usalama wa taifa, Takukuru, ofisi ya
DPP, mkemia mkuu wa serikali, magereza, polisi na kitengo cha kudhibiti
na kupambana na madawa ya kulevya.
Vyanzo vyetu vinasema kuwa katika
mkutano huo, maazimio ya pamoja ni kila idara kutimiza wajibu wake bila
kutazama sura wala nafasi ya mtu ili haki ionekane ikitendeka, huku
ikisisitizwa kesi kuharakishwa na hukumu kutolewa.
No comments:
Post a Comment