Jeshi la Korea Kaskazini leo limekata mawasiliano ya simu na Korea Kusini, na kusitisha mawasiliano ya mwisho ya moja kwa moja baina ya nchi hizo mbili, katika wakati ambapo kuna hofu kubwa ya kijeshi.
Hatua hiyo imechukuliwa sambamba na tangazo kwamba viongozi wakuu wa kisiasa wa Korea Kaskazini watakutana katika siku chache zijazo kujadili kuhusu "suala muhimu" na kufanya uamuzi wa kurudi nyuma. Hatua ya kukata mawasiliano ya simu imetangazwa na afisa wa ngazi ya juu wa jeshi la Kaskazini kwa mwenzake wa kusini muda mfupi kabla ya kukatwa laini hizo za simu. Wiki chache zilizopita, Korea Kaskazini ilikata laini za simu za Shirika la Msalaba Mwekundu ambazo zilikuwa zimetumiwa katika mawasiliano ya kiserikali bila kuwepo uhusiano wa kidiplomasia. Hatua hiyo ya kukatwa mawasiliano ya simu ndiyo ya karibuni katika msururu wa vitisho na hatua kutoka serikali ya Pyongyang na kuongeza hofu katika Rasi ya Korea tangu uzinduzi wa Korea Kaskazini wa kombora la masafa marefu mwezi Desemba na majaribio yake ya nyuklia mwezi uliopita.
No comments:
Post a Comment