Saturday, March 9, 2013

KIBAKA ASULUBIWA BAADA YA KUIBA BETRY YA GARI




 Baada ya kutuhumiwa kuiba Betri ya Gari ndipo wananchi wa eneo la Uyole jijini Mbeya, wakaamua kumfanyia Unyama wa kumtundika juu ya mti kama yesu alivyotundikwa msalabani

 Mkazi wa jijini Mbeya eneo la Uyole akimuliwa na askari Polisi baada ya kutaka kupata kichapo kutoka kwa wananchi baada ya kutuhumiwa kuiba Betri ya gari


HABARI Group YAFANYA HARAMBEE NA KUFANIKIWA KUKUSANYA ZAIDI YA MILIONI SITA


Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki katikati akichangia katika harambee ya kikundi cha Habari Group ambao ni waanishi wa Habari waliojikusanya kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi na pia kuhudumia jamii isiyojiweza kikundi hicho kinaendeshwa chini  ya jumuiya ya kukuza uchumi Ilala 'Jukuila' kikundi hicho kimezinduliwa March 8 Mlezi akiwa ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Angela Kairuki wa pili kulia Udhinduzi huo umedhaminiwa na Mfuko wa Pesheni wa PPF pamoja na Hotel ya Lamaa kushoto ni mratibu wa hafla hiyo Bi, Rabia Bakari  


Mratibu wa Kikundi ya HABARI Group Bi.Rabia Bakari akikabidhi risara ya kikundi hicho wakati wa uzinduzi
Wana kikundi cha Habari Goup wakijitambulisha mbele ya mgeni rasmi

WAANDISHI WA HABARI WA VYOMBO MBALIMBALI VYA HABARI AMBAO NI WANACHAMA WA HABARI Group
WANACHAMA WA HABARI Group WAKICHEZA KWA SHANGWE
Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki kushoto akiangalia baadhi ya dokomenti

picha na www.burudan.blogspot.com

Friday, March 8, 2013

WOMEN'S DAY- SIKUKUU YAPENDEZA MOSHI - KILIMANJARO


UJUMBE WA MWAKA 2013
ASP GRACE LYIMO MGENI WA HESHIMA SIKU YA MWANAMKE DUNIANI MANISPAA YA MOSHI MKOANI KILIMNAJARO
 CHUO KIKUU TUMAINI MAKUMIRA
 
ASP GRACE LYIMO MGENI WA HESHIMA SIKU YA MWANAMKE DUNIANI MANISPAA YA MOSHI MKOANI KILIMNAJARO

TAARIFA KWA VYOMBO YA HABARI MIKAKATI YA KUENDELEZA MPIRA WA MIGUU KWA WANAWAKE


Utangulizi: 

Awali ya yote napenda kuchukua nafasi hii kwa niaba ya kamati ya utendaji ya TWFA kuwashukuru wajumbe wa mkutano mkuu kwa kutupa ridhaa ya kuongoza chama kwa kipindi cha miaka minne.

http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2011/07/Taifa-ladies1.jpg
Pia napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru wadau wote wa mpira wa miguu kwa kutuwezesha kufika hapa tulipo. Napenda niwashukuru wadau wote kwa ujumla wao na pia kuishukuru serikali kwa namna ya pekee zaidi kwa mchango wake ,na mashirika na makampuni ambayo yamekuwa karibu sana nasi NMB, SERENGETI, NSSF, PPF, na Bakheresa Group of Companies.

Tunaamini kabisa kuwa vyombo vya habari ni washirika wetu wakubwa katika kuendeleza mpira wa miguu wanawake. Napenda kuvishukuru vyombo vyote vya habari hapa nchini na hata vile vya nje vilivyoweza kutoa nafasi katika ujenzi wa mpira wa miguu wanawake.

 Maendeleo ya mpira
 Kutekeleza na kuendeleza mpango wa grassroot.

Kwa kushirikiana na Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania,Chama cha Mpira  wa Miguu wanawake  na vyama vya mikoa na wadau mbalimbali  tutaendelea kuendeleza mradi wa mpira wa miguu kwa watoto wa kike na wa kiume Grassroot programme.(umri wa miaka 06-12).kwa mwaka 2013 mradi huu utatekelezwa katika mikoa  mitano (5) mikoa hiyo ni  Tanga,Pwani.Mwanza,Mtwara na Lindi. Mradi huu unaendeshwa kupitia shule za msingi.Kwa mwaka 2012 Mradi huu umeendeshwa katika mkoa wa Dar es Salaam na  watoto wapatao 8766 (wasichana 4909 na wavulana 3857 ) na walimu 26 wameshirikishwa.

Mafunzo ,semina na makongamano
Kwa mwaka 2013 tunatengemea kuendesha mafunzo mbalimbali katika nyanja kuu nne za maendeleo ya mpira wa miguu yaani Utawala na uongozi,Ualimu(Ukocha)  Uamuzi na utabibu katika mpira wa miguu .Katika mwaka mwaka 2013 mafunzo yatafanyika zaidi katika nyanja ya uongozi ili kuwajengea stadi za uongozi viongozi wengi ambao wameingia madarakani katika chaguzi zilizofanyika kwa mwaka 2012/2013.Mafunzo ya utawala na uongozi yatafanyika katika mikoa nane:Dar es Salaam,Pwani,Morogoro,Mwanza,Musoma,Shinyanga,Kilimanjaro na Tanga.Katika mafunzo hayo baadhi ya washiriki watateuliwa kutokana na uwezo wao kwa kuzingatia vigezo vitakavyowekwa na watahudhuria semina itakayo andaliwa kwa kushirikiana na shirikisho la mpira wa miguu Tanzania.

Mafunzo kwa walimu katika ngazi mbalimbali na uratibu wa utekelezaji wa mafunzo yaliyofanyika yatapewa kipau mbele.

Mafunzo kwa waamuzi yatalenga zaidi kuibua vipaji vya watoto wa kike walioko mashuleni na wachezaji wanaomaliza/waliomaliza muda wao.Mafunzo yatafanyika kwa awamu mbili katika mkoa wa Dar es Salaam.

Madaktari  wa michezo  ni muhimu sana katika maendeleo ya mpira na afya za wachezaji kwa kushirikiana na vyombo husika mafunzo kwa mwaka 2013 yatafanyika kwa awamu mbili na yatafanyika katika mkoa wa Dar es Salaam. 
Wanahabari wenye uweledi katika mpira wa miguu wa wanawake ni chachu ya maendeleo ya mpira huo.Nafasi ya wanahabari ni kubwa katika kuendeleza mpira wa miguu ili kuwajengea ujuzi zaidi kutakuwa na mafunzo kwa wanahabari yatakayofanyika Dar es Salaam.

Uongozi na utawala bora
Maendeleo ya mpira wa miguu kwa wanawake yanahitaji viongozi bora na waliopewa ridhaa na vyombo husika.Chaguzi zimefanyika katika  mikoa 16 kati 25  ya mikoa ya Tanzania Bara. Pia tunahimiza mikoa ambayo haijafanya uchaguzi ifanye chaguzi mapema.  Mikoa hiyo ni: Dar es salaam, Mwanza, Kilimanjaro, Rukwa, Arusha, Geita, Simiyu, Njombe, Katavi na Mbeya.

Katika chaguzi hizo kuna baadhi nafasi zote hazikujazwa ni matumaini yetu kuwa  zitajazwa katika mikutano ijayo ya vyama husika.
Pia nichukue nafasi hii kuwahamasisha kina mama wengi wenye sifa kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali katika vyama vya mikoa na taifa pale uchaguzi utakapoitishwa.

Mashindano
Mashindano mbalimbali ndio moyo wa mpira wa miguu bila mashindano  hakuna anayeweza kutambua  ubora na kiwango chakena pia ni kipimo cha maendeleo.
Kutakuwa na mashindano mbalimbali katika ngazi ya  mikoa,taifa na kimataifa.
Mashindano hayo pia yatahusisha shule za msingi na sekondari  na vyuo mbalimbali.Kwa kushirikiana na vyombo husika kutakuwa na ufuatiliaji wa karibu wa michezo ya UMISSETA toka ngazi ya mkoa hadi Taifa na kuwa na mpango endelevu wa kuwaendeleza wale wenye vipaji ambao wamechaguliwa /wanaweza kuchaguliwa kwenye timu za taifa.

Ligi itachezwa katika ngazi za mikoa na baadaye kuunda kombaini ya mkoa itakayoshiriki mashindano ya taifa.

Kwa mwaka 2013 tunatengemea mikoa kuchezesha ligi isiyopungua timu tano kwa mikoa 15 itakuwa na timu  10 na timu itaruhusiwa kusajili wachezaji 25 kwa mwaka 2013 tunatengemea watoto/wasichana  3750 kushiriki katika mpira wa miguu. Idadi hii ukizidisha mara nne unapata jumla ya wachezaji 15,000.Endapo tutakuwa na benki ya wachezaji hawa tutaweza kuunda timu bora za umri tofauti na zenye kiwango cha juu.

Pia mikoa inahimizwa kuanzisha mashindano mbalimbali yatakayoamsha ari kwa watoto wa kike na wasichana kushiriki katika mpira wa miguu.

Uratibu wa mikoa
Wajumbe wa kamati ya utendaji pamoja na  majukumu yao kama wajumbe watakuwa na jukumu la kuratibu shughuli za  maendeleo ya mpira wa miguu katika mikoa:Uratibu huo utakuwa kama ifuatavyo:
Rose Kissiwa
Makamu Mwenyekiti
Tabora, Dodoma, Rukwa, Kigoma, Pwani
Amina Karuma
Katibu
Lindi, Mtwara, Iringa, Njombe, Ruvuma
Zena Chande
Mjumbe
Dar es Salaam, Morogoro, Katavi, Shinyanga, Mbeya
Triphonia Temba
Mjumbe
Manyara, Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Singida
Sophia Charles
Mjumbe
Mara, Kagera, Simiyu, Geita, Mwanza
Kwa mujibu wa katiba ya TWFA  ibara ya 37  inatoa nafasi kwa kamati ya utendaji kuunda kamati ndogo za kuendeleza mpira wa miguu wanawake kamati hizo ni kamati ya Fedha na mipango,kamati ya Ufundi,kamati ya ngingine itakayoonekana inafaa.Kamati ya utendaji kwa pamoja ilikubaliana kuunda kamati ya habari na masoko.
Kamati ya Fedha na Mipango
1.     Rose Kissiwa       - Mwenyekiti
2.     Evans Aveva
3.     Sophia Tigalyoma
4.     Sophia Mukama
5.     Asha Baraka
Kamati ya Ufundi
1.     Tryphonia Temba – Mwenyekiti
2.     Florence Ambonisye
3.     Miraji Fundi
4.     Dr. Leonia Kaijage
5.     Furaha Francis
6.     Richard Muhotoli
Kamati ya Habari na Masoko
1.     Zena Chande – Mwenyekiti
2.     Beatrice Mgaya
3.     Mohamed Mkangara
4.     Florian Kaijage
5.     Somoe Ng’itu

Masoko na Habari
Mpira wa miguu wanawake hauna udhamini na pia vyanzo rasmi vya kupata mapato.Kwa kupitia kamati ya habari na masoko ,tunaamini kutakuwa na mikakakti mbalimbali ya kuelimisha ,kuhamasisha wadau na watanzania wote kuwiwa na kujitoa kuendeleza mpira wa miguu .
  
Asanteni
Lina P.Kessy
Mwenyekiti Chama cha Mpira wa miguu wanawake 

TENGA (RAIS WA TFF) BADO ASISITIZA KUMUONA WAZIRI MICHEZO


RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga amemshukuru Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangara kwa kukubali ombi la Shirikisho la kutaka kukutana naye kwa mazungumzo na kumsihi asitishe hatua anazodhamiria kuchukua hadi hapo kikao hicho kitakapofanyika.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj6xD1QIJTa_XzZLipp5aKZD07zBgfM11QEjH2TsuCebhyDNPL9mqtJHqeIdiZT7onnNsG1RoLFKrwpthmO6zsbXA2_ZkYStLIyPYOl97-V-PSpNytQ3xMmwBD7XqQ2cYhbJnBME_cZYc89/s400/TanzaniaFootballFederation.jpg
Waziri Mukangara ameiagiza TFF kuitisha Mkutano Mkuu wa marekebisho ya katiba ifikapo tarehe 15 Aprili 2013 na Mkutano Mkuu wa Uchaguzi ifikapo tarehe 25 Mei 2013 na kwamba tamko la TFF kutekeleza maagizo hayo liwe limetolewa katika muda wa siku tano zinazoishia Jumatatu (Machi 11, 2013).

Katika barua pepe ambayo amemuandikia Waziri ambaye kwa sasa yuko nje ya nchi, Rais Tenga ameeleza kuwa alikwenda ofisini kwake tarehe 7 Machi 2013 kujaribu kumuona lakini akaambiwa amesafiri, hivyo kuomba kukutana na Katibu Mkuu wa Wizara, ambaye pia hakuwepo ofisini na hatimaye akakutana na Naibu Katibu Mkuu.

Katika barua hiyo pepe, Rais Tenga ameeleza madhumuni ya kutaka kuonana na Waziri Mukangara kuwa ni kwanza “kukushukuru kwa kukubali kuonana na ujumbe wa TFF ulioongozwa na mjumbe wetu wa Kamati ya Utendaji, Bw. Alex Mgongolwa, akiongozana na Katibu Mkuu wa TFF, Bw. Angetile Osiah, jana tarehe 6 Machi 2013.
Tenga, ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu la Afrika (CAF) aliondoka jana (Machi 7 mwaka huu) kwenda Marrakech, Morocco kuhudhuria kikao cha kamati hiyo na pia Mkutano Mkuu wa CAF ambao umepangwa kufanyika Machi 10 mwaka huu ukihusisha pia ajenda ya uchaguzi wa rais.

KAIJAGE AMETEULIWA KUWA KOCHA MPYA TWIGA STARS


ROGASIAN Kaijage ameteuliwa kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya mpira wa miguu ya wanawake, Twiga Stars baada ya kocha wa zamani, Charles Boniface Mkwasa kujiuzulu katikati ya mwaka jana.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjJAut3_IN1k0mtkFGcGglkr70U5yw50dulySAIUwRQwsTan8pZyXRFp_5-3T02xQos180C515FbDuIm1hWnwuZa1QGgCcbi80dal2aaPn2_FzuDA2-mGwz0zPkVCClmH_UZ2XKlSHqma3p/s1600/ROGASIAN+KAIJAGE.JPG
Mkwasa, ambaye alikuwa nyota wa Yanga na Taifa Stars, alijiengua kufundisha timu hiyo aliyoiongoza kwa muda mrefu, baada ya Twiga Stars kuondolewa katika kinyang’anyiro cha kuwania tiketi ya kucheza fainali za Afrika kwa Wanawake (AWC) zilizofanyika nchini Equatorial Guinea.

Twiga ilipata bao muhimu la ugenini jijini Addis Ababa ilipofungwa na wenyeji wao Ethiopia mabao 2-1, lakini ikiwa na matumaini ya kutumia vyema bao la ugenini ilijikuta ikilala bao 1-0 kwenye Uwanja wa Taifa katika mchezo wa marudiano na hivyo kukosa tiketi ya kurudi tena kwenye fainali hizo.

Kaijage ambaye kwa sasa anajihusisha na mradi wa vijana (grassroots) pamoja na programu nyingine za kukuza vipaji zilizo chini ya TFF, aliteuliwa na Kamati ya Ufundi ya TFF kufanya kazi hiyo na ameita kikosi cha Twiga Stars kwa mazoezi ya siku kumi kuanzia Machi 10 hadi 23 mwaka huu Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam.

Wachezaji walioitwa ni Amina Ally (Lord Barden), Asha Rashid (Mburahati Queens), Aziza Mwadini (Zanzibar), Esther Chabruma (Sayari), Esther Mayalla (TSC Academy), Etoe Mlenzi (JKT), Evelyn Sekikubo (Mbarahati Queens), Fatuma Bushiri (Simba Queens), Fatuma Mustafa (Sayari) na Fatuma Omari (Sayari).

Flora Kayanda (Tanzanite), Hamisa Athuman (Marsh Academy), Hellen Maduka (Bujora), Hellen Peter (JKT), Irene Ndibalema (TSC Academy), Maimuna Said (JKT), Mwajuma Abdallah (Tanzanite), Mwanaidi Tamba (Mburahati Queens), Mwanahamis Omari (Mburahati Queens) na Mwapewa Mtumwa (Sayari).

Nabila Ahmed (Marsh Academy), Nasiria Hashim (Zanzibar), Pulkeria Charaji (Sayari), Rukia Khamis (Sayari), Semeni Abeid (Tanzanite), Sharida Boniface (Makongo Sekondari), Sophia Mwasikili (Luleburgaz Gucu Spor, Uturuki), Theresa Yona (TSC Academy), Vumilia Maarifa (Evergreen) na Zena Khamis (Mburahati Queens).

NKAMIA AIPA MBINU SIMBA SC, BAADA YA KUMEGUKA



Aliwahi kuwa katibu mwenezi wa klabu ya Simba ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Kondoa kusini Juma Selemani Nkamia amesema kujiuzulu kwa viongozi wa klabu ya Simba ni pigo kwa klabu hiyo na kwamba kuna haja ya mwenyekiti wa klabu hiyo kutafakari juu ya mustakabali wa klabu hiyo haraka iwezekanavyo.
http://polis.parliament.go.tz/images/Pictures/1625.jpg
Nkamia amesema habari za kujiweka pembeni kwa viongozi hao mjumbe wa kamati ya utendaji ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya usajili ya klabu hiyo Zakharia Hans Poppe na makamu mwenyekiti wa klabu hiyo Geoffrey Nyange Kaburu zimemshitua sana na kwamba huenda kunasababu iliyojificha nyuma ya pazia na kwamba kuna haja ya kuketi chini na kutafakari kwa kina.

Amesema Has Poppe amekuwa na mchangano mkubwa katika klabu ya Simba tangu wakati ule akiwa ni kiongozi wa klabu hiyo na kwamba huenda kuna tatizo kubwa ambalo kiongozi huyo ameliona na kuona bora akae pembeni jambo ambalo linatahitaji tafakari ya kina ya wanachama.
                                                                                                          
Nkamia amesema huenda tatizo likawa ni kwa mwenyekiti wa klabu hiyo kupingana na maamuzi ya vikao halali vya wajumbe wa kamati ya utendaji au kujiamulia mambo yake mwenyewe  hali ambayo huenda ikapelekea wajumbe wengine wakafuata nyayo hizo na kuleta athari kubwa kwa klabu hasa wakati huu ligi ikiwa inaelekea ukingoni.

Aidha amemuomba mwenyekiti wa klabu hiyo Alhaji Ismail Aden Rage kufanya busara kwa kulitazama jambo hili kwa makini sana kwani huenda yeye akawa ndiyo tatizo ndani ya klabu hiyo.

MUGABE ZIARANI AFRIKA KUSINI


Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe yuko ziarani nchini Afrika Kusini kwa mazungumzo na mshirika wake, Jacob Zuma.
 
http://www.thelondoneveningpost.com/africa/wp-content/uploads/2012/05/Mugabe1-640x486.jpg
Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe
Ziara hiyo inafanyika siku chache kabla ya Wazimbabwe kupiga kura kuhusu katiba mpya ya nchi hiyo. Rais Mugabe alihudhuria mkutano wa vyama vya zamani vya ukombozi na mapambano, ulioandaliwa na Rais Zuma mjini Pretoria. Tarehe 16 ya mwezi huu wa Machi, wananchi wa Zimbabwe watapiga kura kuikubali au kuikataa katiba mpya. Aidha, uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika Julai, mwaka huu. Viongozi hao wote wawili wamekataa kujibu maswali kuhusu kura ya maoni kuhusu katiba, licha ya kuwepo madai ya kuyakandamiza mashirika ya kiraia na haki za binaadamu.

Thursday, March 7, 2013

KABURU ATAKA KUJIUZULU SIMBA SC


MAKAMU Mwenyekiti wa Simba SC, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ inadaiwa amemuandikia barua pepe, Mwenyekiti wa klabu hiyo, Alhaj Ismail Aden Rage kumtaarifu kujiuzulu wadhifa huo. 

Habari ambazo JAIZMELALEO imezipata jioni hii zimedai kuwa, Kaburu amemuandikia barua pepe Rage, ambaye kwa sasa yupo India kwa matibabu ya mgongo kumjulisha uamuzi wake huo.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiZC3mR34MdJU7Pgnq2LqxoPASVy3pkTNt06ZTnhs8HWfgD72cTx3To2tb-_O03DxxDnXRcagaTQvyMh9V-bDEC65jsR9Zl-g_C8A3PdMNkzW5mjLxJZECKL-UtxPEdkIYYsEFR0sTYEm4/s1600/kaburu.jpgJuhudi za kumpata Kaburu mwenyewe kuzungumzia habari hizo, hazikufanikiwa kutokana na simu zake zote kutopatikana.

Kaburu anakuwa kiongozi wa pili wa Kamati ya Utendaji ya Simba kujiuzulu leo, baada ya awali mchana, Zacharia Hans Poppe aliyekuwa Mjumbe kujiuzulu pia. 

Hans Poppe, aliyekuwa pia Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, alisema kwamba ameamua kujiuzulu nyadhifa zote hizo kwa sababu kuna mgawanyiko ndani ya uongozi unaokwamisha maendeleo.
CHANZO: BIN ZUBEIRY

WANANCHI WATAKWA KUACHA TABIA YA KUPOKEA AU KUTOA RUSHWA


Wito umetolewa kwa wananchi kote nchini kuacha tabia ya kutoa au kupokea rushwa kwani ni kinyume cha sheria na haki za binadamu ikiwa ni pamoja na kurudisha nyuma maendeleo ya taifa. 

Akizungumzia kuhusu tatizo la rushwa mwezeshaji wa shirika lisilo la kiserikali linaloshughulikia haki za Binadamu na Jinsia Ana Claire Shija  amesema wananchi wanatakiwa kudai haki zao pasipo kutoa au kupokea rushwa ili kuhakikisha vitendo vya rushwa vinatokomezwa kabisa hapa nchini.

Akifafanua zaidi Shija amesema watu wenye hali ngumu kimaisha hasa  wajane ,walemavu ,wanawake na watoto kutokana na kukutana na kusuasua  kimaisha kuwa na uwezo mdogo hali inayowakatisha tamaa na kutokuwa na imani kwa wanaoshughulikia matatizo hayo kwani huwadai rushwa ili waweze kupata msaada.

Kwa upande wa washiriki katika kuitaka serikali kutokomeza vitendo vya rushwa hapa nchini wamesema kuna haja ya serikali kubadilisha sheria zilizozopo tangu kuanzishwa kwa mabaraza hayo ya usuluhishi mwaka 1985 kwani zimepitwa na wakati kutokana na wananchi wengi kutoelewa umuhimu wake.

Hata hivyo wamependekeza kuwa wananchi wapewe elimu itakayowasaidia  kutambua umuhimu wa mabaraza hayo ya mashauri ili kupunguza kesi za migogoro ya ndoa, kazi na ardhi katika mahakama  za mwanzo.

Aidha wamesema changamoto nyingine ni vitendea kazi na mazingira magumu katika mabaraza hayo  na kutopewa motisha jambo linafanya  kutomalizika kwa mashauri mbalimbali.

BAADHI YA WANAFUNZI ST. AUGUSTINE UNIVERSITY WAZUIA MGAMBO KUMCHUKUA MHALIFU

MGAMBO aliyejulikana kwa jina la Abubakari (Ustazi), leo jioni majira ya saa mbili kasoro alizuiliwa na baadhi ya wanachuo wa St. Augustine University of Tanzania, mtaa wa Nyamalango, baada ya kushindwa kujitetea kwa kuonyesha vitambulisho vya kazi yake.

Hayo yalitokea baada ya kutaka kumfunga pingu mwanafunzi wa chuo hicho kwa uthibitisho wa RB ya polisi  yenye nambari 1200 ya mwaka 2013 kwa kosa la kufanyia fujo dada mmoja aliyejulikana mara moja kwa jina la Francisca katika mtaa wa Nyamalango Malimbe Mwanza.

Mwanafunzi huyo alikataa kufungwa pingu hizo baada ya kuwahisi mgambo wale si polisi na kuomba msaada kwa wanafunzi ili aachiliwe ndipo mgambo yule alizidwa nguvu na baadhi ya wanafunzi hao na kuamriwa akae chini ya ulinzi.

Polisi pia walifika katika tukio hilo na kuwachukua mgambo hao mhalifu pamoja na alyefaniwa fujo.


RECORD ZA WANAFUNZI, MGAMBO NA POLISI HIZ HAPA:-


Tuesday, March 5, 2013

AFRICAN LYON KUJUA MUSTAKABALI WAKE CHAMAZI


HATMA ya African Lyon kuendelea kushika mkia au la, kwenye Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inajulikana kesho wakati itakapokuwa mwenyeji wa Ruvu Shooting kwenye Uwanja Azam Complex ulioko Chamazi, Dar es Salaam.

MTEMI RAMADHANI AACHIA NGAZI TFF


Mkurugenzi wa utawala wa shirikisho la soka nchini TFF, Mtemi Ramadhani  hii ametangaza rasmi kuwa sio muajiriwa tena wa shirikisho hilo kutokana na mkataba wake na TFF kuisha.

CHAVEZ HOI KWA MARA NYINGINE TENA


Rais Hugo Chavez wa Venezuela anaripotiwa kuwa na matatizo makubwa  katika mfumo wake wa kupumua wakati akiendelea na tiba ya kemikali, jambo linaloiweka afya yake katika hatari zaidi. 

Sunday, March 3, 2013

SIMBA SC YATOLEWA KLABU BINGWA NA RECREATIVO DE LIBOLO


Wawakilishi wengine wa Bara katika michuano hiyo, Simba SC wametolewa baada ya kufungwa mabao 4-0 na Recreativo de Libolo ya Angola kwenye Uwanja wa Manispaa mjini Calulo, Angola.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj-K9rPd3kVM1mkX-3RKZ0uOpxpZCrUnvbKJXz8kst5348LYllQ7RfjmtOCQVmbt7JjSApkz_pSpze0G5zoJA09HV4LYbdLeaHVPus5fljk-l-zrwzbkFHXltkUrwiYaDGVUHcByrSd-A8/s1600/simba+sc.jpg
Matokeo hayo, yanaifanya Simba itolewe kwa jumla ya mabao 5-0, baada ya