Friday, March 29, 2013

XI JINPING ATUA CONGO BRAZZAVILLE LEO


Rais Xi Jinping wa Jamhuri ya umma wa China amewasili leo Brazaville-mji mkuu wa Jamhuri ya Kongo-kituo cha mwisho cha ziara ya mataifa matatu barani Afrika.

http://www.scmp.com/sites/default/files/styles/980w/public/2013/03/29/china_xi.jpg?itok=VzmjHMGsRais Xi na mkewe Peng Liyuan walipokelewa uwanja wa ndege mjini Brazaville na Rais Denis Sassou Nguesso.Makubaliano yenye thamani ya  mabilioni ya dola yanatarajiwa kutiwa saini wakati wa ziara hiyo ya siku mbili nchini Congo-ya kwanza kufanywa na rais wa China katika nchi hiyo masikini yenye wakaazi milioni nne na rasilmali mali kubwa ya mafuta.Mojawapo ya makubaliano hayo yanahusu ujenzi wa njia kuu yenye urefu wa kilomita 500 kati ya mji mkuu Brazaville na mji mkuu wa kiuchumi ulioko katika mwambao wa bahari ya Atlantik,Pointe-Noire.Baadae hii leo rais Xi Jinping amepangiwa kulihutubia bunge la Jamhuri ya Kongo na kesho atazinduwa hospitali na maktaba mjini Brazaville kabla ya kurejea nyumbani mjini Beijing.Rais wa Jamhuri ya umma wa China,Xi Jinping alianzia ziara yake nchini Tanzania kabla ya kwenda Afrika Kusini alikohudhuria mkutano wa mataifa matano yanayonyanyukia kiuchumi-BRICS.

CHANZO: DPA/RFI

No comments:

Post a Comment