Monday, April 22, 2013

MAHAKAMA YA RUFAA YATUPILIA MBALI RUFAA YA KUPINGA USHINDI WA MBUNGE WA ARUSHA MJINI -CHADEMA GODBLESS LEMA NA KUAMURU WAKATA RUFAA KULIPA GHARAMA ZOTE ZA KESI


Mbunge wa Arusha Mjini-Chadema. Godbless Lema
Ombi la kwanza la waleta rufani la kutaka review ya uamuzi uliotolewa na mahakama ya rufaa juu ya kesi ya Mh.Lema na kutaka isikilizwe na jopo la majaji 7 limetupiliwa mbali leo katika mahakama ya rufaa na sasa ni majaji walewale waliotoa hukumu wamepitia ,Mahakama imetupilia mbali madai ya kwanza kwa kuwa hayapo based on merits Kesi hii ilifunguliwa tena baada ya Mh.Lema kushinda rufaa tarehe 21 desemba 2012,Warufani safari hii walitaka mahakama ipitie upya uamuzi uliotolewa na jopo la majaji watatu na wametaka kuwe na majaji saba.

Mahakama imetupilia mbali mashtaka yao na mahakama imewaamuru tena wakata rufaa walipe gharama zote za kesi.

WAZIRI WA FEDHA ATIA SAINI KITABU CHA WAGENI, UBALOZI, WASHINGTON, DC



 Mhe. Waziri wa Fedha Dkt. Wiliam Mgimwa akitia saini kitabu cha wageni kwenye Ubalozi wa Jamhuri ya Tanzania, Washington, DC Jumamosi April 20, 2013 baada ya Ubalozi kumualika kwenye chakula cha yeye na ujumbe wake.
 Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Lily Munanka akiamuangalia Mhe. Waziri wa Fedha Dkt.  Wiliam Mgimwa akitia saini kitabu cha wageni, Ubalozi wa tanzania nchini Marekani uliopo Washington, DC.
Kutoka kushoto ni Afisa Ubalozi Suleiman Saleh, Mhe. Waziri wa Fedha Dkt. Wiliam Mgimwa, Kaimu Balozi Mhe. Lily Munanka na Afisa Ubalozi Paul Mwafongo katika picha ya pamoja na Mhe. Waziri

SERIKALI YATENGA BILIONI 326 KUWAKOPESHA WANAFUNZI 95,902 WA ELIMU YA JUU NCHINI KWA MWAKA 2012/13.


SERIKALI imetenga shilingi Bilioni 326.0 katika mwaka wa masomo 2012/2013 kwa ajili ya kuwakopesha wanafunzi 95,902 wakiwemo wanafunzi wa mwaka wa kwanza, ikilinganishwa na kiasi cha Shilingi Bilioni 56.1 kilichokuwa kimetengwa mwaka wa masomo 2005/2006 kilichomudu kukopesha wanafunzi 42,729.

1
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,
Mhe. Philipo Mulugo
 Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mhe. Philipo Mulugo wakati akijibu swali la  Mhe. Rashid Ali Abdallah Mbunge Jimbo la Tumbe alilotaka kujua kwanini Serikali imeshindwa kuwapatia mikopo baadhi ya Wanafunzi wenye sifa za kuendelea na masomo na Serikali ina mpango gani wa makusudi kuhakikisha kuwa Wanafunzi hao wanapata elimu.

Alisema kuwa ongezeko hilo la fedha ni ishara tosha kuwa Serikali ina nia ya kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wenye sifa za kusoma Vyuo vya Elimu ya Juu wanapata mikopo itakayowawezesha kupata elimu yao katika mazingira mazuri.

 “Serikali ina nia njema ya kuhakikisha kuwa kila Mtanzania mwenye uwezo wa kusoma Chuo cha Elimu ya Juu anapata fursa hiyo”. Naibu Waziri Mulugo alisema. Aliongeza kuwa kwa mwaka wa masomo 2012/2013, wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliowasilisha maombi ya kupata mkopo walikuwa 37,315, baada ya uchambuzi kufanyika wanafunzi waliobainika kuwa na sifa ya kukopeshwa walikuwa 34,140 lakini kati ya hao ni wanafunzi 30,319 sawa na asilimia 88.9 walipata mikopo.
 
“Kwa mantiki hii wanafunzi waliokosa mikopo ni 3,821 sawa na asilimia 11.1 ya wanafunzi wote walioomba mkopo, wanafunzi hawa wachache walikosa mikopo hiyo kutokana na ukomo wa kibajeti pamoja na vipaumbele vilivyowekwa na Serikali”. Mhe. Mulugo alisema.

Na Benedict Liwenga-Maelezo, Dodoma.

AIRTEL NA KAMPENI ZA 'YATOSHA' HUKO TANGA KWA KISHINDO



Masanii  maarufu kwa vichekesho Masele  wa kundi la vituko shoo toka Dar es salaam akitoa burudani kwa wakazi wa Tanga  wakati wa Tamasha maalum la uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel yatosha katika viwanja vya Tangamano mkoani Tanga
Umati wa wakazi wa Tanga wamejitokeza kushuhudia burudani na kuzindua rasmi huduma ya Airtel yatosha mkoani Tanga katika viwanja vya Tangamano mkoani humo
Wasanii wa kundi la Toto afrika wakionyesha umahiri wao wa kucheza na moto jukwaani wakati wa tamasha maalum la uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel yatosha katika viwanja vya tangamano mkoani tanga mwishoni mwa wiki 
Masanii Erick wa kundi vituko shoo toka Dar es salaam akitoa burudani kwa wakati wa Tamasha maalum la uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel ya Airtel yatosha katika viwanja vya Tangamano mkoani Tanga


Airtel yatosha yatua kwa kishindo mkoani Tanga Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imeendelea na utaratibu wake wa kufanya matamasha ya wazi yenye lengo la kutoa burudani pamoja na kuitambulisha huduma yake mpya ya AIRTEL YATOSHA kwa jamii ambapo mwishoni mwa hii Airtel ilifanya tamasha katika viwanja vya Tangamano
mjini hapo.

 Akizungumza wakati wa Tamasha hilo Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando alisema "Airtel tumefurahishwa sana na umati wananchi wanaojitokeza kwaajili ya burudani lakini pia inatusaidia kuwajulisha wote habari njema za unafuu wa gharama za mawasiliano kupitia huduma yetu ya Airtel YATOSHA Tunawakumbusha kuwa YATOSHA ni huduma ya kudumu na inasaidia sana kupunguza gharama za mawasiliano kwa wateja wetu. 

Kujiunga na huduma hii ili ujipatie vifurushi vya SIKU au WIKI piga *149*99# "Binafsi nimeshangaa na kufurahi sana sana kwa uwepo wa kifushi cha TOSHA cha hadi shilingi 349" na najipatia dakika 25 kuongea bure duuuh!, kweli hii Imetosha!" alisikika akisema Hassan Juma mkazi wa chumba geni mkoani Tanga mara baada ya uzinduzi huo wasanii mbalimbali wa kizazi kipya akiwemo Ney wa Nitego, Nadii, Fid Q, na Juma Nature akiwa na kundi lake walipanda jukwaani kutoa burudani mfululizo huku wananchi waliojitokeza wakifuatia burudani hiyo mwanzo mwisho Kati ya vibao vilivyopigwa na wasanii hao na kuwavutia wakazi wa Tanga ni pamoja na kile cha 'nani kwamwaga pombe yangu kilichoimbwa na Madee toka kundi la Tip Top Connection, wakati wahudhuriaji wa tamasha hilo wengi wao walionekana kuvutiwa zaidi na msanii wa hip hop Ney wa mitego hasa kwa umahiri wake wa kupanga mistari na free style zake alipoachia free style.  
Airtel inaendelea kufanya uzinduzi wa huduma ya airtel yatosha kupitia matamasha ya burudani kwa ambapo baada ya tamasha la Dar es salaam, Morogoro, Chalinze na Tanga kupita airtel yatosha jumamosi na jumapili hii inahamia jijini Mwanza katika viwanja vya Furaisha ambapo wasanii wa bongo flava watatoa burudani bure.

WAZAZI WAHAMASISHA WATOTO WAO KUFELI - KIBONDO MKOANI KIGOMA

UJENZI wa shule za sekondari za kata katika baadhi ya maeneo ya Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma badala ya kuhamasisha jamii kupenda elimu, umesababisha baadhi ya wazazi kuelekeza watoto wao, watoe majibu ya uongo katika mitihani yao ya darasa la saba ili wafeli.

Wazazi hao hawafurahishwi na kuongezeka kwa uhakika wa wahitimu wa darasa la saba kuendelea na kidato cha kwanza, ambao umeelezwa kuwakosesha watoto wao muda wa kufanya shughuli za shamba.

Wakizungumza na gazeti hili katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo, walimu, wanafunzi na viongozi wa serikali, walikiri kuwepo kwa tatizo hilo.

Walitoa mifano ya baadhi ya wazazi waliowahi kuchukuliwa hatua, baada ya kushawishi watoto wao wafeli mitihani. Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Ntoyoyo katika kijiji cha Nyakasanda wilayani Kibondo, Amos Mabula alisema tatizo hilo lipo na limekuwa kikwazo kwa baadhi ya watoto wenye uwezo darasani katika kufanya vizuri kwenye mitihani yao ya kumaliza elimu ya msingi.

Mabula alisema kuwa ana muda mfupi tangu ahamie katika shule hiyo, lakini habari ambazo amezipata kutoka kwa wanafunzi na walimu wenzake ni za wazazi kushawishi watoto wao kujibu vibaya mitihani yao ya mwisho, ili wafeli na kushindwa kuendelea na masomo ya sekondari.

Katika kuthibitisha hilo, Mwalimu Mabula alimwita mmoja wa wanafunzi hao, anayesoma darasa la sita katika Shule ya Msingi Nyakasanda, ambaye alidai wazazi wake wamewahi kufanya jambo hilo kwa dada yake.

Mwanafunzi huyo alidai kuwa dada yake (jina limehifadhiwa) aliyemaliza darasa la saba shuleni hapo mwaka 2011, alifanya vibaya kwenye mitihani ya kumaliza darasa la saba na kushindwa kuendelea na masomo ya sekondari.


Alisema kwa sasa dada yake huyo yuko nyumbani akiwasaidia wazazi wake kazi za vibarua shambani na biashara za mpakani mwa Tanzania na Burundi.

Alidai kuwa dada yake huyo, alikuwa na uwezo darasani na alikuwa akishika nafasi kati ya kwanza na tano na hakuwahi kushuka hapo.

Lakini, alisema mama yao alimwambia dada yake afanye vibaya kwenye mitihani yake ili afeli, kwani hawataweza kumsomesha masomo ya sekondari. Mwaka huo, wanafunzi wanane walifaulu kuendelea na masomo ya sekondari katika shule hiyo, na kumwacha msichana huyo akiwa amefeli. Jambo, hilo liliwashangaza walimu na walipomhoji imekuwaje, alieleza kwamba alipata maelekezo ya wazazi wake kufanya hivyo.


Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mkarazi, Asumwisye Peter, alisema baadhi ya wazazi wamekuwa tatizo kubwa katika kusimamia taaaluma za watoto wao, kwani wazazi wengi katika eneo hilo hawataki watoto wao waendelee na masomo ya sekondari.


Mwalimu Peter alisema aliwahi kukumbana na tatizo hilo katika Shule ya Msingi Nyange na Shule ya Msingi Mabamba, ambako amewahi kufanya kazi, baada ya matokeo ya baadhi ya wanafunzi katika mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka jana kutia shaka.

Alisema katika kutafuta kiini cha kufeli kwa wanafunzi hao walikuwa na uwezo darasani, alimtafuta mmoja wa wanafunzi hao ambaye alimwambia kuwa alifeli kwa sababu alijibu hovyo hovyo kwenye mitihani yake, kama alivyoambiwa na wazazi wake.

Hatua Ofisa Elimu ya Msingi katika Halmashauri ya Wilaya Kibondo, John Kasigwa, amekiri kuwepo kwa tatizo hilo.

Alitoa mfano wa mtihani wa mwaka 2011, ambapo mwanafunzi mmoja alipewa maelekezo ya kufanya hivyo na wazazi wake. Hata hivyo alisema kuwa mwanafunzi huyo alitoa taarifa kwa walimu, ambao waliutaarifu uongozi wa wilaya na mzazi wa mwanafunzi huyo, alikamatwa na kufikishwa Polisi.

Kesi hiyo ilifikishwa pia kwa Mkuu wa Mkoa Kigoma, Issa Machibya. Mkuu wa Wilaya Kibondo, Venance Mwamoto, alisema kuwa tatizo hilo lipo kwa shule za msingi zilizopo katika mwambao wa mpaka wa wilaya hiyo na nchi jirani ya Burundi.

Alisema alishawahi kukumbana na tukio la mwanafunzi ambaye wazazi wake walitaka afanye vibaya kwenye mitihani yake ya kumaliza elimu ya msingi, lakini mwanafunzi huyo alifanya vizuri na kufaulu. Mwamoto alisema mwanafunzi huyo alifika ofisini kwake na kutoa taarifa kuhusu wazazi wake kugoma kumlipia ada, kwa sababu amefaulu kinyume na matakwa yao.

Mkuu huyo wa wilaya alisema tatizo hilo kwa kiasi kikubwa linatokana na mwamko duni wa elimu wa wakazi wengi wa wilaya hiyo, na kwamba anatarajia kuitisha kikao cha wadau wa elimu kuzungumzia changamoto inayoikabili sekta ya elimu katika wilaya hiyo.

Alisema kuwa pamoja na kikao cha wadau wa elimu, pia ataitisha kikao cha viongozi wa dini zote ili wasaidie kuhimiza umuhimu wa elimu ya watoto kwa wakazi wa wilaya hiyo ambao wanapenda kuhudhuria kwenye nyumba za ibada.

Baaadhi ya wananchi na viongozi wa serikali za vijiji wamekiri kuwepo kwa tatizo hilo na kusema kuwa kwa kiasi kikubwa linachangiwa na hali duni ya kipato cha wananchi wa wilaya hiyo na hivyo kutoona umuhimu wa elimu kwa watoto wao kutokana na kuwatumia watoto hao katika shughuli za kiuchumi kwa ajili ya kipato cha familia.
CHANZO:  HABARILEO

WATU 185 WAFA NIGERIA KUTOKANA MAPIGANO BAINA YA BOKO HARAM NA JESHI LA NCHI HIYO


Watu wasiopungua 185 wameuliwa kaskazini mashariki mwa Nigeria katika mapigano kati ya vikosi vya jeshi la nchi hiyo na wapiganaji wa Boko Haram. 

 http://serving.thisdaylive.com/0bef99d6-acf5-4e2c-9779-8fa02ba3fcd4/assets/Boko-Haram-Suspects.jpg?maxwidth=400&maxheight=540
Lewa Kole afisa wa serikali za mitaa amemueleza gavana wa jimbo la Borno Kashin Shettima kuwa mapigano yalianza Ijumaa iliyopita huko Baga katika jimbo la Borno na kudumu kwa masaa kadhaa.

Hata hivyo bado haijafahamika ni askari, raia au wanamgambo wangapi wa Boko Haram waliouliwa katika mapigano hayo kwa kuzingatia kuchomwa moto viwiliwili vingi ambavyo havijaweza kutambuliwa, kufuatia moto ulioteketeza karibu mji huo wote. Brigedia Jenerali Austin Edokpaye amesema kuwa raia wengi walitumiwa na wapiganaji wa Boko Haram kama ngao ya binadamu katika mapigano hayo.