Monday, March 25, 2013

MAHAKA YA JUU KENYA YATAKA KUHESABIWA KURA UPYA VITUO 22


Mahakama ya Juu nchini Kenya imeamuru kura zihesabiwe upya katika vituo 22, kufuatia uchaguzi wa urais ambao uliepuka duru ya pili kwa kura chache.

http://gdb.voanews.com/64D17400-83EA-4EA9-BCB0-535DA270C867_w640_r1_s.jpg

Amri iliyotolewa na jaji wa mahakama hiyo hivi leo, Smokin Wanjila, imetaka kuhesabiwa upya kwa kura katika vituo hivyo, ambavyo ni kama chembe tu ya vituo 32,000 vilivyokuwepo katika uchaguzi wa Machi 4, kuanze kesho.  Pia nayo Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) imetakiwa kuweka wazi daftari la wapiga kura ililotumia kuhesabu kura, baada ya mfumo wa elektroniki kukwama. Matokeo rasmi ya uchaguzi huo yalimpa ushindi Uhuru Kenyatta, ambaye alivuuka mstari wa asilimia 50 kwa kura 8,000 tu. 

Hata hivyo, Kenyatta alimzidi mpinzani wake wa karibu, Raila Odinga, kwa kura 800,000. Muungano wa CORD, unaoongozwa na Odinga, na mashirika kadhaa ya kiraia wamewasilisha kesi katika mahakama ya juu ya Kenya, wakilalamikia kile walichokiita hitilafu kubwa wakati wa uchaguzi.

No comments:

Post a Comment