Wednesday, February 20, 2013

MBOZI YAKABIDHI MAABARA ZINAZOHAMISHIKA NNE KWA SHULE ZA SEKONDARI


 MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA MBOZI LEVISON CHILLEWA AKIMKABIDHI DIWANI WA MSIA MH MAKUNGANYA MOJA YA MEZA ZILIZOTOLEWA KUFUATIA MSAADA WASERIKALI WA KIASI CHA SHILINGI MILION 24 KWA HALMASHAURI ZOTE NCHINI KWAAJILI YA KUBORESHA MAABARA KATIKA SHULE ZA SEKONDARI 

 MMOJA WA WATAALAMU WA MAABARA AKIONYESHA NAMNA ZANA HIZO ZINAVYOFANYA KAZI KABLA YA KUKABIDHIWA KWA WAKUU WA SHULE ZA KATA WALIOONGOZANA NA MADIWANI WAO

 MIONGONI MWA SHULE ZA KATA ZENYE UHITAJI WA VIFAA NA MAABARA AMBAPO KWA MIAKA TAKRIBANI SITA WATOTO WAMEKUWA WAKISOMA BILA KUFANYA MAZOEZI YA VITENDO 

 AFISA ELIMU SEKONDARI WILAYA YA MBOZI BWANA ISAACK MGAYA AKIPEWA MKONO WA SHUKRANI NA BAADHI YA WALIMU NA DIWANI WA KATA YA RUANDA BAADA YA SHULE YA LUMBILA KUPEWA MEZA YA MAABARA INAYPOTEMBEA

 MIONGONI  MWA ZANA ZITAKAZOGAWIWA MASHULENI KWAAJILI YA KUIMARISHA MAFUNZO KWA VITENDO
OFISA KATIKA IDARA YA ELIMU SEKONDARI AKIONYESHA NAMNA YA KUUNGANISHA  MFUMO WA MAJI KWENYE MEZA YA MAABARA


HALMASHAURI ya wilaya Mbozi imekabidhi meza nne za maabara inayotembea kwaajili ya mafunzo ya vitendo katika masomo ya Baiolojia, Kemia , Kilimo na Fizikia kwa shule nne za sekondari ikiwa ni sehemu ya hatua za kukabili changamoto za matokeo mabaya ya shule za sekondari katika masomo ya sayansi.

Afisa Elimu sekondari wilayani Mbozi bwana Isaack Mgaya, amesema meza hizo zenye thamani ya shilingi Milion 24 zinatokana na msaada uliotolewa na serikali mwezi juni wa kiasi hicho cha fedha kwaajili ya kuziwezesha shule za sekondari kuwa na Maabara zinazohamishika.

Amesema hatua hiyo inaziwezesha shule Mbili za sekondari kwa wilaya mpya ya Momba za Mkulwe na Nkangamo kuwa na maabara wakati kwa upande wa wilaya ya Mbozi shule za sekondari za Msia na Lumbila pia zimenufaika.

Bwana Mgaya amesema Mobile Laboratory kama zinavyofahamika zimebuniwa ili kuwezesha kukidhi mafunzo ya masomo ya sayansi kwa vitendo katika shule za sekondari na Vyuo.

Aidha alifafanua kuwa matumizi yake yanawezesha madarasa hayo kuhama hama kulingana na mahitaji na kwamba pia zinaweza kutumika chini ya miti, ama maeneo yasiyo na mifumo ya umeme ama maji hivyo kurahisisha uelewa wa wanafunzi kulingana na mazingira waliyopo

kwa upande wake mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Wilaya ya Mbozi bwana Levison Chilewa ambaye aliambatana na Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Momba Bwana Juma Kitabuge ameeleza kuwa kutokana na muundo wa maabara hizo, madiwani wa kata zilizonufaika na mpango huo wanapaswa kujenga hoja za kushawishi madiwani wenzao ili kutenga kiwango kikubwa cha fedha za mapato ya ndani ya halmashauri hizo mbili kwaajili ya ununuzi wa meza hizo ambazo zitakuwa mkombozi kwa watoto katika masomo ya sayansi.

Alisema hivi sasa wanafunzi wamekuwa waoga wa masomo hayo kutokana na mazingira ya kusomea kutokuwa yenye mvuto ikiwa ni pamoja na kukosekana kwa zana muhimu na maabara, na kwamba hatua ya kusambazwa kwa teknolojia hiyo rahisi kunawawezesha wanafunzi sasa kujifunza katika hali iliyobora zaidi kwa vitendo.

Alisema ni vyema pia kwa shule zilizo karibu kuona namna ambavyo zinaweza kushirikiana kutumia maabara moja kwa kutembeleana hatua ambayo itarahisisha katika ufundishaji na hata kuleta tija katika matumizi ya maktaba hizo badala ya kuazimisha meza hizo kutoka shule moja kwenda shule nyingine hali ambayo inaweza kusababisha uharibifu.

Akizungumzia msaada huo, diwani wa kata ya Ruanda bwana Keneth Mgala amesema, kimsingi hatua hiyo itasaidia kupunguza hali ya matokeo mabaya kwenye masomo ya sayansi ambapo wanafunzi wakti mwingine wanalaumiwa kwa kuonewa kutokana na mazingira yenyewe ya shule kukosa vitu muhimu kama maabara hivyo kushindwa kuhamisha nadharia katika vitendo ama kuoanisha vyote viwili.

Kwa kipindi kirefu,Shule pekee yenye maabara ya kubuniwa na utundu wa mwalimu mmoja wilaya ya Mbozi ipo katika shule ya sekondari ya Vwawa ambapo maaabara hiyo imekuwa  shule kadhaa zimekuwa zikitembelea na  kujifunza ubunifu huo kwa lengo la kwenda kutengeneza katika shule zingine ili kuongeza hamasa ya  wanafunzi kupenda masomo ya sayansi
Kwa hisani ya Danny Tweve wa Indaba blog.

SERIKALI YA BULGARIA YAJIUZULU


 Serikali ya Bulgaria imejiuzulu kufuatia kufanyika maandamano ya nchi nzima kupinga hatua za kubana matumizi na kupanda kwa gharama za umeme.

http://cdn.24.co.za/files/Cms/General/d/2301/8018bc03bc444e7dbd43add7e44dc4ab.jpgWaziri Mkuu wa Bulgaria Boiko Borisov ametangaza taarifa hiyo hivi leo na kuliambia bunge la nchi hiyo kuwa hawezi kuendelea kuwa ndani ya serikali ambayo jeshi la polisi linawapiga wananchi. Borisov amesema kuwa wao kama viongozi wana utu na heshima na wanatambua kuwa ni wananchi ambao wameiweka serikali madarakani lakini anashangaa kuona hivi leo serikali inawanyanyasa raia hao. Bulgraia ni nchi mwanachama wa Umoja wa Ulaya ambayo ina umasikini mkubwa. Imekumbwa na wimbi la maandamano la wananchi wanaolalamikia hali ngumu ya maisha.

KAWAMBWA APEWA SIKU 14 KUJIUZULU WADHIFA WAKE


CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimetoa muda wa siku 14 Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa, na Naibu wake, Philip Mulugo, kuhakikisha wamejiuzulu nyadhifa zao.

Kauli hiyo ya CHADEMA imetolewa na mwenyekiti wake taifa, Freeman Mbowe, wakati alipokuwa akihutubia mkutano mkubwa wa hadhara, uliofanyika jana katika viwanja vya Furahisha Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, ikiwa ni ufunguzi wa Baraza la Viongozi wa CHADEMA, Kanda ya Ziwa Magharibi.

Mbowe ambaye aliongoza maandamano makubwa ya magari na pikipiki kuelekea uwanjani hapo, alisema, Kawambwa, naibu wake, Mulugo, pamoja na katibu mkuu wa wizara hiyo, wameshindwa kuiongoza sekta hiyo muhimu, ndiyo maana kwa sasa wanafunzi wanaishia kuandika matusi na kupata sifuri katika mitihani ya kuingia kidato cha kwanza.
http://www.ippmedia.com/media/picture/large/Kawambwa(13)(1).jpg
Dr. Shukuru Kawambwa.

Alisema waziri huyo lazima ajiuzulu nafasi hiyo, kwani taifa ameliingiza pabaya na kuanza kuzalisha maelfu ya watoto wa maskini kumaliza elimu zao za msingi na sekondari wakiwa hawajui kusoma na kuandika.

Mbowe alisema hili ni janga la kitaifa, hivyo lazima Kawambwa aondoke ndani ya wiki mbili, vinginevyo CHADEMA itaitisha maandamano makubwa nchi nzima kushinikiza kiongozi huyo ang’oke madarakani.
CHANZO: TANZANIA DAIMA

Sunday, February 17, 2013

PAKISTAN YAOMBOLEZA VIFO VYA WATU 81 KWA BOMU


Idadi ya vifo kufuatia shambulizi kubwa la bomu lililofanywa dhidi ya Waislamu wa madhehebu ya Shia kusini magharibi ya Pakistan imepanda leo na kufikia watu 81.
http://farm8.staticflickr.com/7273/7712266466_3b7736014a_z.jpg
Wakaazi wa eneo hilo wametishia kufanya maandamano ikiwa hakuna hatua madhubuti itakayochukuliwa dhidi ya waliofanya shambulio hilo. Bomu hilo lililokuwa na takribani tani moja ya miripuko, na kufichwa ndani ya tangi la maji, liliripuka jana jioni, katika soko moja lillokuwa limejaa watu katika mji wa Hazara, ambao unakaliwa na waislamu wengi wa Kishia. Eneo hilo liko karibu na Quetta; mji mkuu wa mkoa wa Baluchistan. Afisa mkuu wa polisi eneo hilo amesema idadi ya waliojeruhiwa imefika watu 178. Mkoa wa Baluchistan umeendelea kukumbwa na mashambulizi za kimadhehebu baina ya waislamu wa madhehebu ya Sunni walio wengi nchini humo, na washiya ambao wanajumlisha moja juu ya tano ya jumla ya watu milioni 180 nchini Pakistan. Shambulizi hilo la Jumamosi limefanya idadi ya mauwaji ya mashambulizi la kimadhehebu mwaka huu nchini Pakistan kufikia 200, ikilinganishwa na zaidi ya 400 waliouawawa mwaka wa 2012, mwaka ambao Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch liliztaja kuwa mbaya zaidi dhidi ya Washiya nchini humo.

TENGA AWAASA WALIOENGULIWA KUFUATA TARATIBU

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga amewataka waombaji uongozi ambao hawaridhiki na uamuzi wa Kamati ya Rufani ya Uchaguzi kutafuta haki yao kwa mujibu wa taratibu zilizopo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam jana (Februari 16 mwaka huu) mchana, Rais Tenga amesema  TFF ni moja ya taasisi ambazo zina utaratibu unaoeleweka kwa wadau wake.

“Wote tunafahamu taratibu ambazo tumejiwekea juu ya wagombea wetu wanachaguliwaje. TFF ni moja ya taasisi ambazo zina utaratibu unaoeleweka. Hii ni kuanzia wilayani. Kama kuna tatizo zipo njia za kufuata.

“Katika mchakato wa uchaguzi wengine wanafanikiwa, wengine wanaachwa. Wameachwa kwa sababu zilizotolewa na Kamati ya Rufani ya Uchaguzi. Ambaye haridhiki anafuata taratibu tulizojiwekea. Atafute haki yake kwa mujibu wa taratibu,” amesema.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEim7lRrOsYHfZYKdrdHvRjG70mbmp1v3z69HvtW4gOmOTuakY87p9nsKiJO9cJATVq2vyKjPLNSaIQvcvFJbcYu8fj3LNNYuW3WQ0GHRKhmBfh7_VFZhRTaRSF3x4BU_ZO2xZP3LX8BKDY/s640/Tenga+wa+TFF.jpgRais Tenga amesisitiza kuwa kikatiba hana uwezo wa kuingilia uamuzi unaofanywa na kamati ambazo ameziunda, kwani utawala bora ni kusimamia kanuni ambapo wanaofanya uamuzi lazima waweke wazi sababu za uamuzi waliofikia.

Amesema ambao hawakubaliani na uamuzi wa Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF dhidi yao wana njia tatu za kufuata. Njia hizo ni kuiomba Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ipitie uamuzi iliofanya (review), kuandika Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kuomba liingilie au kwenda Mahakama ya Usuluhishi ya Michezo (CAS).

“Hata ukiweka ngazi nne, mtu akiathirika ataona ameonewa tu. Kwa Katiba yetu hapa (Kamati ya Rufani ya Uchaguzi) ndiyo mwisho. Hakuna chombo kingine. Ukiwaomba FIFA waingilie, watakuja na tutawaeleza mchakato wote ulivyokwenda. Tunapenda kuwahakikishia hawa (waathirika) kuwa kwa maslahi ya mpira wa miguu tutasaidia katika hilo wapate haki,” amesema Rais Tenga na kuongeza kuwa tayari waathirika wawili wa uamuzi wa Kamati ya Rufani ya Uchaguzi wameomba marejeo (review) kwenye kamati hiyo hiyo.

Amesema TFF imelazimika kuzungumzia suala hilo kwa sababu limekuwa likizungumzwa kinazi zaidi wakati taratibu ziko wazi, hivyo kwa maslahi ya mpira wa miguu ni vizuri taratibu zikafuatwa.

“Nawaomba washabiki wa mpira wa miguu, tumejenga chombo hiki (TFF) kwa muda mrefu. Bado tunaomba watu watusaidie, kwa hiyo matusi hayawezi kubadili kitu. Tunachowahakikishia ni kuwa, mtu anapoomba msaada tutampa kutafuta haki yake.

“Hizi ni kamati huru, lazima ziheshimiwe. Ukianza kuziingilia utakuwa umeua mpira wa miguu. Uongozi ni utumishi, tusionekane tunagombana. Huu si ubunge, mbunge anachaguliwa anakwenda kulipwa mshahara. Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF halipwi mshahara. Tusirudi kwenye matusi, tulishaondoka huko,” amesema.

Kuhusu mabadiliko ya Katiba yaliyofanyika kwa njia ya waraka, Rais Tenga amesema yamefanyika kwa mujibu wa taratibu, na haikuwa siri. Maeneo yaliyofanyiwa marekebisho ilikuwa ni lazima, kwani mengi yalikuwa ni maagizo kutoka FIFA na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).

Amesisitiza kuwa mabadiliko hayo yamefuata taratibu na hakuna udanganyifu katika hilo, kwani ridhaa ya kutumia waraka iliombwa, na Mkutano ni watu ambao ndiyo wamepitisha mabadiliko hayo.

“Mkutano Mkuu ni watu, si kikao. Katika dunia ya leo mikutano inafanyika kwa tele conference, si lazima watu wakutane sehemu moja,” amesema na kuongeza kuwa mabadiliko hayo yalipitishwa kwa kura 70 dhidi ya 33 zilizokataa.

Kuhusu Kanuni kusainiwa kabla ya Katiba, Rais Tenga amesema tarehe ya kuanza kutumika Katiba ni siku ridhaa ilipopatikana, na si siku mhuri wa Msajili ulipopigwa. Mabadiliko ya Katiba yalipita Desemba 15 mwaka jana, Kanuni zilisainiwa Januari 7 mwaka huu.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

MAKABU NA NEFZI WAJIGAMBA KWA WAPINZANI WAO


Yale mapambano mawili ambayo yalikuwa yanasubiriwa kwa hamu kubwa sana katika bara la Afrika yamefanyika katika majiji mawili ya Johennsburg, Afrika ya Kusini na Tunis, Tunisia baada ya kuibuka miamba miwili katima ubingwa na uzito tofauti!
 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgV0IWxs6sEOEkRND3-GeNLTu43_C3JMb0SydNsSKcg9w-dNj7b9ytv8khV_WQklIeu6Xw8nOhWSo7XQahKF9iu2ok7fGsRwJodDr3oww73kAegyKHdCJkLaVVFF6pnoksZfEOrP4ops1UW/s1600/IMG_0641%5B1%5D.JPG
Katika jiji la Johannesburg nchini Afrika ya Kusini, Mkongo man Ilunga Makabu alimchakaza bila huruma bondia Gogito Gorgiladze kutoka nchini Georgia kwa TKO katika raundi ya nne (4)!

Mawili hao walikuwa wanagombea ubingwa wa dunia wa vijana walio chini ya miaka 25 katika uzito wa