Mkurugenzi wa utawala wa shirikisho la soka nchini TFF, Mtemi Ramadhani hii ametangaza rasmi kuwa sio muajiriwa tena wa shirikisho hilo kutokana na mkataba wake na TFF kuisha.
Mtemi ambaye ni mchezaji wa zamani wa Simba SC, amesema ameifanyia kazi TFF kwa miaka minne na sasa anaona na muda muafaka wa kuachia nafasi hiyo kwa mtu mwingine na yeye aendelee kujishughulisha ujasiriamali mwingine.
"Nimeitumikia TFF vizuri sana kwa miaka minne iliyopita, mkataba wangu umeisha jana tarehe 3 mwezi tatu. Nimeamua kuendelea na vitu vingine kuachia wengine wapeleke jahazi mbele. Umri wangu umeenda na nafikiri ni muda sahihi wa kujishughulisha na vitu vingine." - alisema Mtemi Ramadhani

No comments:
Post a Comment