MGAMBO aliyejulikana kwa jina la Abubakari (Ustazi), leo jioni majira ya saa mbili kasoro alizuiliwa na baadhi ya wanachuo wa St. Augustine University of Tanzania, mtaa wa Nyamalango, baada ya kushindwa kujitetea kwa kuonyesha vitambulisho vya kazi yake.
Hayo yalitokea baada ya kutaka kumfunga pingu mwanafunzi wa chuo hicho kwa uthibitisho wa RB ya polisi yenye nambari 1200 ya mwaka 2013 kwa kosa la kufanyia fujo dada mmoja aliyejulikana mara moja kwa jina la Francisca katika mtaa wa Nyamalango Malimbe Mwanza.
Mwanafunzi huyo alikataa kufungwa pingu hizo baada ya kuwahisi mgambo wale si polisi na kuomba msaada kwa wanafunzi ili aachiliwe ndipo mgambo yule alizidwa nguvu na baadhi ya wanafunzi hao na kuamriwa akae chini ya ulinzi.
Polisi pia walifika katika tukio hilo na kuwachukua mgambo hao mhalifu pamoja na alyefaniwa fujo.
RECORD ZA WANAFUNZI, MGAMBO NA POLISI HIZ HAPA:-
No comments:
Post a Comment