Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe yuko ziarani nchini Afrika Kusini kwa mazungumzo na mshirika wake, Jacob Zuma.
Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe |
Ziara hiyo inafanyika siku chache kabla ya Wazimbabwe kupiga kura kuhusu katiba mpya ya nchi hiyo. Rais Mugabe alihudhuria mkutano wa vyama vya zamani vya ukombozi na mapambano, ulioandaliwa na Rais Zuma mjini Pretoria. Tarehe 16 ya mwezi huu wa Machi, wananchi wa Zimbabwe watapiga kura kuikubali au kuikataa katiba mpya. Aidha, uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika Julai, mwaka huu. Viongozi hao wote wawili wamekataa kujibu maswali kuhusu kura ya maoni kuhusu katiba, licha ya kuwepo madai ya kuyakandamiza mashirika ya kiraia na haki za binaadamu.
No comments:
Post a Comment