Tuesday, March 5, 2013

CHAVEZ HOI KWA MARA NYINGINE TENA


Rais Hugo Chavez wa Venezuela anaripotiwa kuwa na matatizo makubwa  katika mfumo wake wa kupumua wakati akiendelea na tiba ya kemikali, jambo linaloiweka afya yake katika hatari zaidi. 

http://static.guim.co.uk/sys-images/Guardian/Pix/pictures/2013/2/14/1360803224006/Hugo-Chavez-Venezuela-can-009.jpg

Rais Hugo Chavez wa Venezuela 

 
Waziri wa mawasiliano wa nchi hiyo, Ernesto Villegas, alisema katika taarifa iliyosomwa kutoka hospitalini alikolazwa Chavez, kuwa kiongozi huyo amepatwa na maambukizi mapya na mabaya zaidi, na hivyo kuhatarisha mfumo wake wa kupumua.Taarifa hiyo imekuja wiki mbili baada ya Chavez kuwasili katika hospitali ya kijeshi mjini Caracas, baada ya miezi kadhaa ya matibabu nchini Cuba, ambako alifanyiwa upasuaji wa nne wa saratani tangu Julai 2011. Villegas alisema Chavez anaendelea na tiba kali ya kemikali na tiba nyingine, na kusisitiza kuwa hali yake inazidi kuwa mbaya.

No comments:

Post a Comment