MAKAMU Mwenyekiti wa Simba SC, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ inadaiwa amemuandikia barua pepe, Mwenyekiti wa klabu hiyo, Alhaj Ismail Aden Rage kumtaarifu kujiuzulu wadhifa huo.
Habari ambazo JAIZMELALEO imezipata jioni hii zimedai kuwa, Kaburu amemuandikia barua pepe Rage, ambaye kwa sasa yupo India kwa matibabu ya mgongo kumjulisha uamuzi wake huo.
Juhudi za kumpata Kaburu mwenyewe kuzungumzia habari hizo, hazikufanikiwa kutokana na simu zake zote kutopatikana.
Kaburu anakuwa kiongozi wa pili wa Kamati ya Utendaji ya Simba kujiuzulu leo, baada ya awali mchana, Zacharia Hans Poppe aliyekuwa Mjumbe kujiuzulu pia.
Hans Poppe, aliyekuwa pia Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, alisema kwamba ameamua kujiuzulu nyadhifa zote hizo kwa sababu kuna mgawanyiko ndani ya uongozi unaokwamisha maendeleo.
CHANZO: BIN ZUBEIRY
No comments:
Post a Comment