Wito umetolewa kwa wananchi kote nchini kuacha tabia ya kutoa au kupokea rushwa kwani ni kinyume cha sheria na haki za binadamu ikiwa ni pamoja na kurudisha nyuma maendeleo ya taifa.
Akizungumzia kuhusu tatizo la rushwa mwezeshaji wa shirika lisilo la kiserikali linaloshughulikia haki za Binadamu na Jinsia Ana Claire Shija amesema wananchi wanatakiwa kudai haki zao pasipo kutoa au kupokea rushwa ili kuhakikisha vitendo vya rushwa vinatokomezwa kabisa hapa nchini.
Akifafanua zaidi Shija amesema watu wenye hali ngumu kimaisha hasa wajane ,walemavu ,wanawake na watoto kutokana na kukutana na kusuasua kimaisha kuwa na uwezo mdogo hali inayowakatisha tamaa na kutokuwa na imani kwa wanaoshughulikia matatizo hayo kwani huwadai rushwa ili waweze kupata msaada.
Kwa upande wa washiriki katika kuitaka serikali kutokomeza vitendo vya rushwa hapa nchini wamesema kuna haja ya serikali kubadilisha sheria zilizozopo tangu kuanzishwa kwa mabaraza hayo ya usuluhishi mwaka 1985 kwani zimepitwa na wakati kutokana na wananchi wengi kutoelewa umuhimu wake.
Hata hivyo wamependekeza kuwa wananchi wapewe elimu itakayowasaidia kutambua umuhimu wa mabaraza hayo ya mashauri ili kupunguza kesi za migogoro ya ndoa, kazi na ardhi katika mahakama za mwanzo.
Aidha wamesema changamoto nyingine ni vitendea kazi na mazingira magumu katika mabaraza hayo na kutopewa motisha jambo linafanya kutomalizika kwa mashauri mbalimbali.
No comments:
Post a Comment