Friday, March 29, 2013

PICHA MBALIMBALI ZIKIMUONESHA RAIS KIKWETE AONGOZA MAMIA KUUAGA MWILI WA MBUNGE WA CHAMBANI DAR ES SALAAM LEO


 Kaimu Katibu wa Bunge Mhe John Joel akisoma wasifu wa marehemu





 Rais jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Spika Anne Makinda alipowasili katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo Machi 29, 2013 kuongoza waombolezaji katika kuuaga mwili wa Mbunge wa Chambani(CUF),Salim Hemed Khamis aliyeanguka ghafla jana katika Vikao vya kamati ya Bunge na kufaikiri katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Baada ya shughuli hii mwili ulisafirishwa kuelekea Chambani, Pemba, kwa maziko.
 Rais jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Mbunge wa Monduli Mhe Edward Lowassa na Mbunge wa Mafia Mhe Abdulkarim Shah alipowasili katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo Machi 29, 2013 kuongoza waombolezaji katika kuuaga mwili wa Mbunge wa Chambani(CUF),Salim Hemed Khamis aliyeanguka ghafla jana katika Vikao vya kamati ya Bunge na kufaikiri katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Baada ya shughuli hii mwili ulisafirishwa kuelekea Chambani, Pemba, kwa maziko.
 Rais jakaya Mrisho Kikwete akitia saini kitabu cha maombolezo katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo Machi 29, 2013 na kuongoza waombolezaji katika kuuaga mwili wa Mbunge wa Chambani(CUF),Salim Hemed Khamis aliyeanguka ghafla jana katika Vikao vya kamati ya Bunge na kufaikiri katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Baada ya shughuli hii mwili ulisafirishwa kuelekea Chambani, Pemba, kwa maziko.
 Mama Salma Kikwete akitia saini kitabu cha maombolezo  katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo Machi 29, 2013 ambapo Rais Kikwete aliongoza waombolezaji katika kuuaga mwili wa Mbunge wa Chambani(CUF),Salim Hemed Khamis aliyeanguka ghafla jana katika Vikao vya kamati ya Bunge na kufaikiri katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Baada ya shughuli hii mwili ulisafirishwa kuelekea Chambani, Pemba, kwa maziko.
 Wabunge wanawake wakiwa katika maombolezo  katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo Machi 29, 2013 ambapo Rais Kikwete aliongoza waombolezaji  kuuaga mwili wa Mbunge wa Chambani(CUF),Salim Hemed Khamis aliyeanguka ghafla jana katika Vikao vya kamati ya Bunge na kufaikiri katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Baada ya shughuli hii mwili ulisafirishwa kuelekea Chambani, Pemba, kwa maziko.
 Rais jakaya Mrisho Kikwete akiwa na viongzi wa kitaifa na wabunge katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo Machi 29, 2013 ambako aliongoza waombolezaji katika kuuaga mwili wa Mbunge wa Chambani(CUF),Salim Hemed Khamis aliyeanguka ghafla jana katika Vikao vya kamati ya Bunge na kufaikiri katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Baada ya shughuli hii mwili ulisafirishwa kuelekea Chambani, Pemba, kwa maziko.

KOREA YA KASKAZINI YAELEKEZA MAKOMBORA MAREKANI NA KOREA YA KUSINI


Korea ya Kaskazini inasema imeyatega makombora yake ya kimkakati kuelekea Marekani na Korea ya Kusini.

http://si.wsj.net/public/resources/images/WO-AN202_KIM_G_20130328184120.jpgShirika la habari la Korea ya Kaskazini KCNA limemnukuu Rais Kim Jong Un akisema pindi pakitokea uchokozi kutoka Marekani,vikosi vya Korea ya Kaskazini vitalazimika kuishambulia Marekani pamoja na vituo vyake vya kijeshi vilivyoko katika visiwa vya bahari ya Pasifiki,Guam na Hawaii na vile vilivyoko Korea ya Kusini.Kim Jong Un ameamua hivyo kufuatia kutumwa na Marekani  madege mawili  chapa B-2 yenye uwezo wa kubeba makombora ya nuklea hadi Korea ya Kusini hapo jana.Waziri wa ulinzi wa Marekani Chuck Hagel amewaambia waandishi habari katika makao makuu ya wizara ya ulinzi-Pentagon- mjini Washington kwamba Marekani inazingatia kwa makini onyo lililotolewa na kwamba iko tayari kukabiliana na hali yoyote itakayojitokeza.

ULINZI WAIMARISHWA KIPINDI CHA PASAKA

POLISI imesema imeimarisha ulinzi kwenye maeneo yote ya kuabudia na maeneo mengine yenye mikusanyiko katika kipindi chote cha Sikukuu ya Pasaka, inayoanza kuadhimishwa leo kwa ibada ya Ijumaa Kuu.

http://api.ning.com/files/TdIQzJmQRty7mnDQTkaEpx2*gZfH6*A3BWKAB2kj23IE3p8KfjmezlnG-8gTkclBbMd8SZ6OXd5wt14iId0h6KyXzGpZRTVa/advera.jpg
Aidha, Polisi imewataka wananchi kuondoa hofu na kuwapuuza watu wachache, ama kikundi cha watu wanaotumia kipindi hiki cha sikukuu, kuwatia hofu kwa kusambaza ujumbe mfupi wa maneno wenye vitisho kwa watu mbalimbali kwa lengo la kuvuruga amani na utulivu.

Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Senso katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, alisema kitendo hicho cha kusambaza ujumbe ni uhalifu kama uhalifu mwingine na wakibainika hatua za kisheria, zitachukuliwa dhidi yao.

Senso alisema Polisi imejipanga kikamilifu kuimarisha usalama wa raia na mali zao kwa kipindi chote cha sikukuu, kwa kuwataka wananchi kusherehekea kwa amani na utulivu kuazia leo hadi Aprili mosi.

Alisema uzoefu unaonesha baadhi ya watu hutumia kipindi cha sikukuu, kufanya matukio ya uhalifu kutokana na mikusanyiko hiyo ya watu katika maeneo mbalimbali.

Wakati huo huo Polisi imewataka wamiliki wa kumbi za starehe, kuhakikisha usalama na kuzingatia uhalali na matumizi yake katika uingizaji wa watu kulingana na uwezo wake.

Wazazi pia wametakiwa kuwa makini na watoto hasa katika disko toto kuepuka ajali na matukio mengine yanayoweza kusababisha madhara juu yao. Wakati huo huo Ibada ya Ijumaa Kuu kitaifa, inafanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Usharika wa Dodoma Mjini.

Ofisa Habari wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Mchungaji John Kamoyo alisema kuwa Ibada hiyo itaongozwa na Askofu wa Dayosisi ya Dodoma, Amon Kinyunyu. Ibada ya Misa ya Sikukuu ya Pasaka, itafanyika Jumapili katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Paulo wa Msalaba mjini Dodoma.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Idara ya Mawasiliano wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Anatoly Salawa, ibada hiyo itaongozwa na Askofu wa Jimbo la Dodoma, Mhashamu Gervas Nyaisonga.

XI JINPING ATUA CONGO BRAZZAVILLE LEO


Rais Xi Jinping wa Jamhuri ya umma wa China amewasili leo Brazaville-mji mkuu wa Jamhuri ya Kongo-kituo cha mwisho cha ziara ya mataifa matatu barani Afrika.

MKUTANO WA WAANDISHI WA HABARI NA KAMISHINA WA POLISI ZANZIBAR


MAKAO  MAKUU YA POLISI ZANZIBAR
29.03.2013
Ndugu waandishi wa habari,
Assallam Aleykum
Najua leo ni siku ya mapumziko na siku ya ibada kwa waumini wote. Leo tupo katika Ijumaa Kuu lakini pia ni siku ya sala ya pamoja kwa Waislam katika misikiti mbalimbali. Nimeamua tukutane leo kwa sababu tatu. Kwanzza kwa kuendelea kudumisha doria za mjini na vijijini kwa kutumia gari, Askari wa migu, pikipiki na mbwa ili kuhakikisha usalama unadumu Visiwani hapa. Tunaendelea kutoa ushauri wa kiusalama na kushirikiana kwa karibu zaidi na wananchi wote kuona maisha na mali zao zinakuwa salama. Tunawaomba wenye mahoteli ya kitalii na nyumba za starehe kuwa karibuna jeshi lao la Polisi  pamoja na kufuata ushauri wote wa kiusalama wanaopewa kila wakati.
Pili tumeitana hapa kutoa shukurani kwa wananchi wote. Jeshi la Polisi linawashukuru wananchi wote kwa ujumla wao kwa ushirikiano mkubwa mnaotupa. Si rahisi kutaja kila msaada tunaopata kutoka makundi mbalimbali ya wananchi wteu, lakini tukiri msaada tunaopata ni mkubwa na umetusaidia na unaendelea kutusaidia katika kudumisha amani na utulivu. Hata hivyo, napenda kutoa shukurani zangu za dhanti kwa nyinyi waandhishi wa habari hasa wa ahapa Zanzibar kwa kuwa karibu na ofisi yang na kuchangia kwa kiwango kikubwa mchakato mzima wa kudumisha amani Visiwani hapa.
Jambo la tatu tuliloitania hapa ni kupeana taarifa juu ya maendelea ya kesi ya mauaji ya Padri Evarest Mushi. Najua si nyinyi tu waandishi wa habari lakini Watanzania wote wanatka kujua maendeleo ya upelelezi wa tukio hili. Jeshi la Polisi liliwaahidi litawajulisha kila hatua iliyofikiwa juu ya upelelezi wa shauri hili. Mpaka hapa tunapozungumza upelelezi wa shauri hili umefikia pahala pazuri na jalada la shauri hili limeshapalekwa kwa Mkurugenzi wa Mashitaka kwa hatua za kisheria. Muhusika wa mauaji haya tayari amekamatwa na ametambuliwa na watu walioshuhudia tukio hilo. Mtakumbuka Jeshi la Polisi mbali na hatua kadhaa za kiupelelezi walizozichukua ilikuwa ni pamoja na kuchora michoro ya sura ya mtu kwa kutumia  watu walioshuhudia tukio hilo. Baada ya kuitoa picha hiyo katika vyombo vya habari mablimbali vya kiulinzi, wananchi, vyombo vya habari na mitandao ya kijamii muhalifu hyo ametambulika na kutambuliwa.
Marehemu padre Evarist Mushi
Marehemu padre Evarist Mushi
Jeshi la Polisi liliahidi kutoa milioni kumi kwa watu watakaosaidia kupatikana kwa muhalifu huyo. Ahadi ile ipo pale pale na mwananchi aliyesaidia kutoa utambuzi Jeshi la Polisi litamzawadia kiwango hicho cha fedha, laini kwa usalama wa shahidi huyo na kwa sababu za kiupelelezi tukio la kumkabidhi fedha hizo hatutaliweka bayana katika vyombo vya habari.
Jeshi la Polisi linaendelea kuwaomba wananchi kutoa ushirikiano wa hali ya juu ili kufanikisha upelelezi wa matukio mengine yaliyopita. Tunawaahidi kuendelea kuwasisitiza na kutotoa siri wala kuwataja wale wote wanaotupa taarifa za kihalifu.
Mwisho kabisa, naomba niwashukuru tena wananchi wote wa Zanzibara kwa kuwa karibu na ofisi yangu na Jeshi la Polisi kwa ujumla katika mapambano ya vitendo vya kihalifu.
Ahsanteni.
Ijumaa karimu.
MUSSA A. MUSSA – CP
KAMISHNA WA POLISI
ZANZIBAR.

Thursday, March 28, 2013

WANARIADHA 300 WATHIBITISHA KUSHIRIKI MBIO ARUSHA APR 12


JUMLA ya wanariadha wapatao 300 wameshathibitisha kushiriki mbio za kumbukumbu za kifo cha hayati Waziri Mkuu na mpambanaji wa uhuru wa nchi hii, Edward Moringe Sokoine ambazo zinatarajiwa kufanyika Aprili 12 wilayani Monduli, Mkoani Arusha.


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgr5Y46BMjxH0pdKxaRbA1YUuWOFPE8wQWFqYOTO0m2sLV4zfA1cQtqCP7Mt3hhQ6PYZaoY8kcyOXOKH1QjhNZU4aQ5wGFDIHbHCo34LCnXVBaYbTMTWmeGb7Oz81wMWWgyXgH31oC-AAw/s1600/561482_419895221389529_204105510_n.jpg
Wanariadha kutoka katika mikoa ya, Kilimanjaro, Manyara, Tanga, Dar es salaam na Arusha wameshathibitisha kushirki katika mbio hizo za kwanza kufanyika katika historia ya nchi hii tangu uhuru.

Hayo yamebainishwa na mratibu wa mbio hizo ambaye pia ndiye mwongozaji wa mbio hizo, Wilhelm Gidabuday akizungumza,  kwa njia ya simu kutoka Dar es salaam na kusema kwamba tayari kupitia ofisi za chama cha Riadha mkoa Arusha (ARAA), wamethibitisha kushiriki mbio hizo.

Gidabuday alisema kuwa kujitokeza kwa wanariadha hao ni ishara nzuri kwani pamoja na kwamba ndio mara ya kwanza, kwa muitikio huo, wanatarajia kuwa na washiriki zaidi ya 500.

Kuhusu zoezi la usajili, Gidabuday alisema kuwa zoezi hilo litaanza mapema baada ya sikuukuu za Pasaka kumalizika na kuongeza kuwa zoezi hilo litafanyikia katika Ofisi za ARAA, zilizoko katika uwanja wa mpira wa miguu wa Sheikh amri Abeid jijini Arusha kwa ada ya sh. 2000 za Tanzania.

Sokoine Marathon inatarajia kukukutanisha watu wa kada mbalimbali, wakiwemo viongozi, wabunge, mawaziri na wananchi kwa ujumla kuadhimisha kumbukumbu ya kifo cha Hayati Waziri Mkuu wa Tanzania, Edward Moringe sokoine yatakayofanyika Aprili 12, wilayani Monduli katika kijiji alichozaliwa na kuzikwa.

Mbio hizo za umbali wa Kilomita 10 na kilomita 2 kutembea na kukimbia maandalizi yake kwa mujibu wa Waratibu wake mpaka sasa zimeshafikia hatua nzuri na kwa mujibu wa Waratibu wake, hatua zinazofanyika ni kufanya mazungumzo na Mgeni Rasmi ambaye kuna uwezekano akawa mmoja wa viongozi wakuu wa taifa hili.

Mwandishi: FADHIL ATHUMAN
Mhariri: JOHNSON JABIR

MMBUNGE SALIM HEMED KHAMIS KUPITIA TIKETI YA CUF - CHANBANI ZANZIBAR, AMEFARIKI DUNIA


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ITV Tanzania, imesema Mbunge kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF) aliyeanguka jana (Machi 27, 2013) katika mojawapo ya Kamati inayosimamiwa na Waziri Mkuu aliyejiuzulu Edward Lowassa, amefariki dunia baada ya kukimbizwa  hospitalini.

 

Mbunge wa Chambani Salim Hemed Khamis amefariki katika Hospitali ya Muhimbili alikokimbizwa jana na kupelekwa moja kwa moja katika Chumba cha Wagonjwa wanaohitaji uangalizi wa karibu(ICU).

CHANZO: ITV