Sunday, January 6, 2013

NIGERIA YAAMUA KUACHANA NA AMEOBI



Shola Ameobi
Shirikisho la Soka la Nigeria limefunga muda wake wa kumtaka Shola Ameobi anayechezea klabu ya Newcastle kuthibitisha kama atakwenda na kikosi cha Timu ya Taifa hilo nchini Afrika Kusini katika michuano ya AFCON 2013.

Itakumbukwa kwamba jana katika michuano yaFA nchini Uingereza alitolewa kwa kadi nyekundu huku Newcastle wakitolewa katika mzunguko wa tatu wa michuano hiyo maarufu nchini Uingereza. Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 31 alicheza miezi miwili iliyopita na timu yake ya Taifa dhidi ya Venezuela  na kuonekana kuwa ana mchango kwenye timu ya taifa hilo. Shirikisho la Soka nchinihumo lilimpa muda wa kuthibitisha mpaka jana Jumamosi kama anaweza kuchezea timu hiyo ya Taifa katika AFCON hata hivyo hakuweza kuthibitisha kufanya hivyo, bila kutoa sababu yoyote ya msingi. 

Michuano ya Mataifa ya Afrika AFCON nchini Afrika Kusini kuanzia Januari 19 hadi Februari 10.

No comments:

Post a Comment