Jalala likifanyiwa Usafi |
Baadhi ya wakazi wa Sanya juu wilyani Siha mkoani Kilimanjaro wametaka mkandarasi wa kuzoa taka katika maeneo ya Sanya mjini na mitaa yake kutoa huduma hiyo kila siku
Wakazi hao wametoa malalamiko hayo kwa nyakati tofauti walipokuwa wakizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni. Wamesema mkandarasi huyo hivi sasa anazoa taka hizo kila baada ya wiki moja wakati mwingine hata zaidi na kusababisha mlundikano mkubwa wa taka zinazozagaa hovyo hadi kwenye makazi ya watu.
Mkazi moja amesema amechoshwa na kero ya harufu ya taka zinazozaga baada ya kutelekezwa, haswa sehemu yanapouzwa maembe kenye soko la sanya juu na sehemu ya mtaro wa kupitisha maji machafu ambapo umeota majani na mrundikano wa taka zinazotupwa na watu na kutishia kufukiwa kabisa kama hautafanyiwa usafi.
Akijibu malalamiko hayo Bibi Afya wa Wilaya ya Siha Joys Temu amekiri kuwepo kwa taka hizo nakusema kuwa atalifanyia kazi jambo hilo kabla halijaleta hatari kwa wanachi wa maeneo hayo
No comments:
Post a Comment