Mabingwa watetezi wa Kombe la Mataifa ya Afrika Zambia wamejikuta wakinyukwa tena mechi ya tatu mfululizo na timu ya taifa ya Angola ambayo watakutana kwenye michuano hiyo siku chache zijazo kwa mabao 2-0.
Mchezaji wa Angola anayechezea Klabu ya Daraja la Pili nchini Brazil katika klabu ya Parana Geraldo alitupia bao la kuongoza katika dakika ya 8 ya mchezo huo uliochezwa katika uga wa Dobsonville na baada ya dakika 5 yaani dakika ya 13 ya mchezo Mlinzi Amaro anayechezea daraja la kwanza alizifumania nyavu na mabao hayo kudumu hadi dakika 90 za mchezo.
Zambia itaanza kampeni zake Januari 21 na timu ya Ethiopia mechi itakayochezwa katika mji wa Nelspruit ulio Kaskazini Mashariki mwa Afrika Kusini.
Itakumbukwa kwamba Zmabia ilipoteza michezo yake miwili ilipokutana na Saudia na Taifa Stars.
No comments:
Post a Comment