Tuesday, April 30, 2013

ZIARA YA DKT.SHEIN,WILAYA YA KUSINI UNGUJA - ZANZIBAR



 Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa akizungumza na wananchi na wanachama wa Tawi la CCM Mzuri wilaya ya Kusini Unguja,alipofanya ziara ya kuimarisha Chama leo.
 Vijana wa CCM katika Kijiji cha Bwejuu,wakiimba wimbo maalum wa kumkaribisha Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein,alipotembelea katika Tawi la CCM la Kijiji hicho akiwa katika ziara ya kuimarisha Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kusini Unguja leo.
 Baadhi ya wananchi na wanachama wa Tawi la CCM Bwejuu kaskazi wakimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa akizungumza wakati alipotembelea Tawi lao akiwa katika ziara ya kuimarisha Chama katika Mkoa wa Kusini Unguja leo.
 Wanachama wapya wa CCM wakilakiapo cha Utii kwa Chama cha Mapinduzi baada ya kukabidhiwa kadi zao za Chama na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein,alipofanya ziara ya kuimarisha Chama katika Wilaya ya Kusini Unguja leo.
Baadhi ya wananchi na wanachama wa Tawi la CCM Bwejuu kaskazi wakimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa akizungumza wakati alipotembelea Tawi lao akiwa katika ziara ya kuimarisha Chama katika Mkoa wa Kusini Unguja leo. [Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.

KILICHOTOKEA KATI YA REAL MADRID NA DORTMUND


KERO YA FOLENI DAR ES SALAM YAWA KERO


Monday, April 22, 2013

MAHAKAMA YA RUFAA YATUPILIA MBALI RUFAA YA KUPINGA USHINDI WA MBUNGE WA ARUSHA MJINI -CHADEMA GODBLESS LEMA NA KUAMURU WAKATA RUFAA KULIPA GHARAMA ZOTE ZA KESI


Mbunge wa Arusha Mjini-Chadema. Godbless Lema
Ombi la kwanza la waleta rufani la kutaka review ya uamuzi uliotolewa na mahakama ya rufaa juu ya kesi ya Mh.Lema na kutaka isikilizwe na jopo la majaji 7 limetupiliwa mbali leo katika mahakama ya rufaa na sasa ni majaji walewale waliotoa hukumu wamepitia ,Mahakama imetupilia mbali madai ya kwanza kwa kuwa hayapo based on merits Kesi hii ilifunguliwa tena baada ya Mh.Lema kushinda rufaa tarehe 21 desemba 2012,Warufani safari hii walitaka mahakama ipitie upya uamuzi uliotolewa na jopo la majaji watatu na wametaka kuwe na majaji saba.

Mahakama imetupilia mbali mashtaka yao na mahakama imewaamuru tena wakata rufaa walipe gharama zote za kesi.

WAZIRI WA FEDHA ATIA SAINI KITABU CHA WAGENI, UBALOZI, WASHINGTON, DC



 Mhe. Waziri wa Fedha Dkt. Wiliam Mgimwa akitia saini kitabu cha wageni kwenye Ubalozi wa Jamhuri ya Tanzania, Washington, DC Jumamosi April 20, 2013 baada ya Ubalozi kumualika kwenye chakula cha yeye na ujumbe wake.
 Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Lily Munanka akiamuangalia Mhe. Waziri wa Fedha Dkt.  Wiliam Mgimwa akitia saini kitabu cha wageni, Ubalozi wa tanzania nchini Marekani uliopo Washington, DC.
Kutoka kushoto ni Afisa Ubalozi Suleiman Saleh, Mhe. Waziri wa Fedha Dkt. Wiliam Mgimwa, Kaimu Balozi Mhe. Lily Munanka na Afisa Ubalozi Paul Mwafongo katika picha ya pamoja na Mhe. Waziri

SERIKALI YATENGA BILIONI 326 KUWAKOPESHA WANAFUNZI 95,902 WA ELIMU YA JUU NCHINI KWA MWAKA 2012/13.


SERIKALI imetenga shilingi Bilioni 326.0 katika mwaka wa masomo 2012/2013 kwa ajili ya kuwakopesha wanafunzi 95,902 wakiwemo wanafunzi wa mwaka wa kwanza, ikilinganishwa na kiasi cha Shilingi Bilioni 56.1 kilichokuwa kimetengwa mwaka wa masomo 2005/2006 kilichomudu kukopesha wanafunzi 42,729.

1
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,
Mhe. Philipo Mulugo
 Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mhe. Philipo Mulugo wakati akijibu swali la  Mhe. Rashid Ali Abdallah Mbunge Jimbo la Tumbe alilotaka kujua kwanini Serikali imeshindwa kuwapatia mikopo baadhi ya Wanafunzi wenye sifa za kuendelea na masomo na Serikali ina mpango gani wa makusudi kuhakikisha kuwa Wanafunzi hao wanapata elimu.

Alisema kuwa ongezeko hilo la fedha ni ishara tosha kuwa Serikali ina nia ya kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wenye sifa za kusoma Vyuo vya Elimu ya Juu wanapata mikopo itakayowawezesha kupata elimu yao katika mazingira mazuri.

 “Serikali ina nia njema ya kuhakikisha kuwa kila Mtanzania mwenye uwezo wa kusoma Chuo cha Elimu ya Juu anapata fursa hiyo”. Naibu Waziri Mulugo alisema. Aliongeza kuwa kwa mwaka wa masomo 2012/2013, wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliowasilisha maombi ya kupata mkopo walikuwa 37,315, baada ya uchambuzi kufanyika wanafunzi waliobainika kuwa na sifa ya kukopeshwa walikuwa 34,140 lakini kati ya hao ni wanafunzi 30,319 sawa na asilimia 88.9 walipata mikopo.
 
“Kwa mantiki hii wanafunzi waliokosa mikopo ni 3,821 sawa na asilimia 11.1 ya wanafunzi wote walioomba mkopo, wanafunzi hawa wachache walikosa mikopo hiyo kutokana na ukomo wa kibajeti pamoja na vipaumbele vilivyowekwa na Serikali”. Mhe. Mulugo alisema.

Na Benedict Liwenga-Maelezo, Dodoma.