![]() |
| Goldie Harvey |
Friday, February 15, 2013
MSANII MAARUFU WA NIGERIA (GOLDIE HARVEY) AMEFARIKI DUNIA
Msanii maarufu wa kinigeria na aliyekua mshiriki wa Big Brother Africa House of Talent Goldie Harvey amefariki Dunia.
Msanii huyu alizaliwa Susan Filani, na amefariki alhamisi usiku, katika hospitali ya Roddington iliyopo katika kisiwa cha Victoria-Lagos Nigeria.
RAIS KIKWETE, MWINYI NA MKAPA WASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU LAIZER
![]() |
| Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka shada la Maua katika kaburi la Marehemu Askofu Dkt.Thomas Laizer wakati wa mazishi yaliyofanyika katika Kanisa KKKT Usharika wa mjini Kati,Arusha mjini leo. |
![]() |
| Rais Dkt,Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe wakati wa Mazishi ya Skofu Thomas Laizer leo katika kanisa la KKKT Usharika wa mjini Kati |
NSSF YAANDAA MPANGO WA KUONDOA UMASKINI
Mfuko wa hifadhi ya jamii hapa nchini(NSSF)umesema kuwa kwa sasa unaandaa mpango maalumu ambao utalenga kuondokana na Umaskini wa Nchi ya Tanzania huku mpango huo pia ukiongeza ufanisi wa masuala mbalimbali kama vile Ajira na Vipato vya wananchi
Hayo yameelezwa leo mjini Arusha na Mkurugenzi mkuu wa mfuko huo Dkt Ramadhani Dau wakati akiongea na wadau wa mfuko katika mkutano wa tatu unaoendea mjini Arusha.
SAYARI MPYA (2012 DA 14) KUPITA KARIBU NA DUNIA LEO USIKU
Usiku wa leo, sayari ndogo itaikosakosa dunia kwa umbali wa kilomita 27,000.
Sayari hiyo iliyopewa jina la 2012 DA 14 ina kipenyo cha mita 68, na uzito wa tani laki nne itapita karibu na dunia saa nne na dakika ishirini na tano kwa saa za Afrika Mashariki, hii ikiwa ni kwa mujibu wa shirika la anga la Ulaya, ESA.
Thursday, February 14, 2013
Monday, February 11, 2013
BREAKING NEWS
Habari zilizopo ni kuwa leo Geita mapigano yametokea kati ya Waislamu na Wakristo (particular Protestants wa AIC). Na hii ni baada ya Wachungaji wa AIC kutenga eneo la Buselesele kwa ajili ya machinjio ya Wakristo wao,maeneo ya Katoro na jirani ni vurugu na mtifuano!
ASKOFU MSARIKIE KUZIKWA FEB 14 MOSHI
Askofu Mstaafu Amedeus Msarikie wa Jimbo Katoliki Moshi, aliyefariki dunia hivi karibuni, anatarajiwa kuzikwa kwenye Kanisa kuu la Kristu Mfalme, Jimbo Katoliki Moshi, hapo tarehe 14 Februari 2013.
Subscribe to:
Posts (Atom)



