Friday, February 15, 2013

NSSF YAANDAA MPANGO WA KUONDOA UMASKINI

Mfuko wa hifadhi ya jamii hapa nchini(NSSF)umesema kuwa kwa sasa unaandaa mpango maalumu ambao utalenga kuondokana na Umaskini wa Nchi ya Tanzania huku mpango huo pia ukiongeza ufanisi wa masuala mbalimbali kama vile Ajira na Vipato vya wananchi

Hayo yameelezwa  leo mjini Arusha na Mkurugenzi mkuu wa mfuko huo Dkt Ramadhani Dau   wakati akiongea na wadau wa mfuko katika mkutano wa tatu unaoendea mjini Arusha.

http://api.ning.com/files/MaRQ-WguFhYcQDlRuYVREsJeLj6zMnnpWXohHZgQBrIdh0ZnFSxsQAMVk304ehln6exLNnxwX9Z4AaUeEOcvVVFoQ1seOrZL/tnssf.jpg
Dkt Ramadhani amesema kuwa Mfuko huo mpaka sasa umeshaweka Misingi mbalimbali ya kuimarisha zaidi mpango huo wa maendeleo ambapo utaweeza kuraisisha shughuli mbalimbali za kijamii ikiwa ni pamoja na kupambana na Umaskini mkubwa sana hapa nchini.
Aidha amesema kuwa Mpango huo ambao utaanza hivi karibuni pia utaweza kugusa njaja mbalimbali kwenye jamii hasa nyanja ya uwekezaji wa huduma za msingi kwa Mtanzania kwani utafiti uliofanywa na Mfuko huo umebaini kuwa uwekezaji nao unachangia sana kuimarisha hata uchumi wa Nchi

Hata hivyo mbali na hayo amesema kuwa hata Mapato ya mfuko huo nayo yameongezeka sana tofauti na kipindi cha mwaka 2001 ambapo Mapato yake yalikuwa ni bilioni 39 lakini kwa sasa wamefanikiwa kuvuka katika kiwango cha juu sana hadi kufikia kiwango cha Bilioni 500 kwa mwaka hali ambayo inahitajika kuendeleza mipango na mikakati mbalimbali ya  kupambana na Umaskini.

No comments:

Post a Comment