SAYARI MPYA (2012 DA 14) KUPITA KARIBU NA DUNIA LEO USIKU
Usiku wa leo, sayari ndogo itaikosakosa dunia kwa umbali wa kilomita 27,000.
Sayari hiyo iliyopewa jina la 2012 DA 14 ina kipenyo cha mita 68, na uzito wa tani laki nne itapita karibu na dunia saa nne na dakika ishirini na tano kwa saa za Afrika Mashariki, hii ikiwa ni kwa mujibu wa shirika la anga la Ulaya, ESA.
Afisa wa shirika la anga la Marekano, NASA, Donald Yeomans amesema hawana wasiwasi juu ya sayari hiyo.Hakuna uhusiano kati ya sayari hiyo na vimondo vilivyoripuka nchini Urusi.
No comments:
Post a Comment