Friday, February 15, 2013

MSANII MAARUFU WA NIGERIA (GOLDIE HARVEY) AMEFARIKI DUNIA

Msanii maarufu wa kinigeria na aliyekua mshiriki wa Big Brother Africa House of Talent Goldie Harvey amefariki Dunia.

Goldie Harvey
Msanii huyu alizaliwa Susan Filani, na amefariki alhamisi usiku, katika hospitali ya Roddington iliyopo katika kisiwa cha Victoria-Lagos Nigeria.



Kutokana na gazeti la Daily Times, limeandika kuwa msanii huyo amefariki mapema baada ya kutoka kushiriki tuzo za Grammy. (Grammy Awards).

Goldie and Prezzo
Itakumbukwa pia kua msanii huyo alikua pia mshiriki wa Big Brother 2012 ambapo huko aliweza kufahamiana na Msanii maarufu wa Kenya Prezzo. Na kuweza kujenga uhusiano wa kimapenzi
Pia Jumannen ya wiki hii Prezzo aliweza kuzungumzia uhusiano wao na kusema kuwa wamafikia hatua ya kutangaza mipango kufunga ndoa na matangazo hayo yalitarajiwa kurushwa na kituo cha M-Tv.


No comments:

Post a Comment