RAY C ambaye amekiri kwamba sasa angalau amepona na anaendelea
vizuri ametoa ushuhuda mzito kuhusu sakata lake la dawa za kulevya.
Rehema Chalamila (Ray C) |
“Awali sikujua ni wanaume wachache wanaoingia
kwenye uhusiano wa mapenzi ya kweli waliobaki ni kwa faida zao,
nilipopata matatizo ndiyo nikagundua kuna wanaume wanawatumia wanawake
kwa faida yao, kama si uhusiano, inawezekana nisingekuwa Ray C huyu
unayezungumza naye, ambaye inabidi apambane na unene, atafute pumzi ya
kuimba upya. Lakini uhusiano wa kimapenzi na mwanamume niliyeamini
ananipenda ndiyo ulionifikisha hapa bila kujua.”
“Wasichana hasa maarufu wawe makini na wapenzi
wanaoishi nao bila kujali wameishi nao kwa muda gani, wengi wao ni
chanzo cha kufeli kwao kimaisha. Nilikuwa nafanya kazi Nairobi napata
Sh.10 milioni kwa mwezi, zote ziliishia kwenye dhambi.
??Kwa tamaduni za Kiafrika wanawake tunawasikiliza
wanaume, tunaonyesha unyenyekevu kwao, kumbe wakati mwingine
wanatuingiza katika majanga. Sitaki kumtaja aliyeniingiza katika hii
dhambi, lakini ni mpenzi wangu niliyempenda na alifanya hivyo bila mimi
kujua.
Nawataka hata vijana wa kiume wawe makini na
uvutaji sigara au bangi, kwani wakati mwingine wanachanganyiwa na dawa
za kulevya na matokeo yake wanakuwa mateja.
“Wauza bangi wengi wao wanauza unga, wakikuona ni
mteja wao wa kudumu na hubwii unga wanakuchanganyia katika bangi na
matokeo yake unajikuta huwezi kuvuta bangi bila unga. Hivyo unakuwa teja
bila kukusudia kama mimi nilivyochanganyiwa na mpenzi wangu katika
sigara ya kawaida na kujikuta nakuwa teja.
“Sasa wawe makini, hili halina mmoja licha ya
baadhi yao kuwa chanzo cha kuwaingiza wasichana, lakini baadhi yao
wanaweza kujikuta wanaingia huko kwa njia hiyo au kwa kugongeana sigara,
yaani unamkuta rafiki yako anavuta na wewe unaomba akubakizie sasa kama
alitia unga na wewe unaathirika.”
Msanii huyo alipoulizwa kuhusu mapenzi alisema;
“Sina na nitakaa sana na hata nikiwa naye nitakuwa makini kwani
nimeshang’atwa na nyoka kila nikiguswa na unyasi nashituka.”
No comments:
Post a Comment