Sherehe kubwa zaidi ambapo rais wa Ufaransa Francois Hollande amealikwa zitafanyika baadaye mwezi huu.
Wanajeshi wa Ufaransa walisaidia jeshi la Mali
kupambana na wapiganaji wa kiisilamu waliokuwa wameteka eneo la
Kaskazini mwa nchi hiyo mapema mwaka huu.
Mtangulizi wa Keita ambaye kwa sasa ni kaimu
rais, Dioncounda Traore, alisema mnamo Jumatatu kuwa tayari amekabiliana
na changamoto kubwa sana ikiwemo kuandaa uchaguzi wa amani na kuweza
kudhibiti maeneo yaliyokuwa yametekwa na waasi.
Duru zinasema kuwa bwana Keita atastahili kukabiliana na maswala muhimu zaidi kama vile kuleta uthabiti katika eneo la Kaskazini na kuleta mageuzi katika jeshi pamoja na kupambana na ufisadi.
No comments:
Post a Comment