Wednesday, September 4, 2013

PICHA MBALIMBALI KUHUSU MATUKIO YA MAZISHI YA ASKOFU KULOLA

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha waombolezaji wakati wa mazishi ya Askofu Moses Kulola leo.
Mtoto wa Marehemu Askofu Kulola, Willy Moses Kulola (kushoto) akiwa amesimama nyuma ya jenza la mwili wa marehemu baba yake.

 

Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa (kushoto) akishiriki ibada ya mazishi ya Askofu Kulola.

Katibu Mkuu wa Chadema, Dkt Wilbroad Slaa (wa tatu kulia), na mkewe Josephine Mushumbusi (wa pili kulia) wakifuatilia ibada ya mazishi iliyoendeshwa na Askofu Mkuu Msaidizi wa Kanisa la EAGT, Asumwisye Mwaisabila (hayupo pichani).


Mjane wa Marehemu Askofu Kulola, Elizaberth Moses Kulola anayefuta machozi (wa pili kutoka kushoto) akiwa pamoja na ndugu na jamaa wakati wa ibada ya mazishi iliyofanyika nje ya Kanisa la EAGT Calvary Bugando.


Kada maarufu wa CCM, Charles Masalakulangwa naye alikuwa ni miongoni mwa waombolezaji.



Mmoja wa wachungaji waliohudhuria mazishi ya Marehemu Askofu Moses Kuloa, akifuatilia jambo. 
Mchungaji huyo alizua minong'ono kutokana na kufanana na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.



Wajukuu wa marehemu Askofu Moses Kulola wakiimba huku wakiwa wamelizunguka jeneza la mwili wa marehemu babu yao.



Jeneza la mwili wa marehemu Askofu Moses Kulola likishushwa kaburini.



Askofu Mkuu Msaidizi wa EAGT, Asumwisye Mwaisabila akiweka udongo kaburini kuashiria safari ya mwisho ya Marehemu Askofu Moses Kulola.




Mjane wa marehemu Elizabert Moses Kulola, akiweka udongo kwenye kaburi la mumewe huku akisaidiwa na ndugu zake.

Rais Jakaya Kikwete, akiweka udongo kwenye kaburi la Askofu Kulola.

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa akiweka udongo kwenye kaburi la Askofu Kulola.

No comments:

Post a Comment