Jitihada
za kurejesha heshima kwa viwanja vya ndege nchini zilizoanzishwa na
waziri wa uchukuzu Dk. Harisson Mwakyembe zinaonekana kuzaa matunda
baada ya mwanadada kutoka nchini Nigeria Anthonia Ojo (25) kukamatwa na
kete 99 za madawa ya kulevya dar es salaam leo.
|
HUYO NDO ANTHONIA OJO AKIWA KITUO CHA POLISI |
|
Zifuatazo
ni picha mbalimbali za tukio zima la kunaswa kwa mtuhumiwa huyo ambapo
anashikiliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi wakati kete hizo zimepelekwa
kwa ofisi ya Mkemia Mkuu kwa uchunguzi zaidi.
Anthonia
Ojo (25) Raia wa Nigeria akiwa na kete 99 za madawa ya kulevya baada ya
kukamatwa kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA)
Dar es Salaam jana, akieleke Roma Italia kupitia Paris Ufaransa kwa
ndege ya Ethiopian Airways. Msichana huyo aliingia hapa nchini Agosti 30
akitokea Nigeria. Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Viwanja vya Ndege,
Renatus Chalya, Ojo anaendelea kubaki chini ya ulinzi wa polisi kwa
uchunguzi zaidi, wakati madawa hayo yamepelekwa kwa ofisi ya mkemia Mkuu
wa Serikali ili kubaini aina ya dawa hizo, thamani yake na hatimaye
atafikisha mahakamani.
|
AKIZITOA KWENYE MIKEBE YA POWDER NA SHAMPOO |
|
HILO NDO BEGI MADAWA HAYO YALIKUWEMO |
|
SEHEMU YA KETE 99 ALIZOKAMATWA NAZO. |
|
PASPORT YAKE |
|
ANTHONIA OJO AKIWASILI KITUO CHA POLISI CHA JNIA BAADA KUKAMATWA. |
|
ANTHONIA OJO AKIELEKEA KWENYE GARI BAADA YA KUKAMATWA |
|
MADAWA HAYO YAKIRUDISHWA KWENYE VYOMBO BAADA YA KUONESHWA KWA WANAHABARI. |
|
RECORD ZA ANTHONIA ALIWAHI KUJA TENA MWAKA 2011 |
No comments:
Post a Comment