MELI iliyosajiliwa nchini Tanzania ya MV Gold Star juzi Ijumaa
imekamatwa nchini Italia ikiwa na dawa za kulevya zenye thamani ya pauni
milioni 50 sawa na shilingi bilioni 126. 5. Watuhumiwa waliokuwa ndani
ya meli hiyo waliamua kuichoma moto ili kupoteza ushahidi na kuamua
kupiga mbizi majini lakini walitiwa nguvuni na wanausalama wa Italia.
|
MV Gold Star ikiungua baada ya kuchomwa moto na wasafirishaji wa madawa ya kulevya. |
Meli hiyo ya mizigo ilikuwa imepakia tani 30 za madawa na ilikamatwa jirani na Kisiwa cha Sicilia katika Bahari ya Mediterranian nchini Italia wakati ikielekea Uturuki. Maofisa wa polisi nchini humo wamedai kuwa watuhumiwa tisa waliokamatwa ni raia wa Misri na Syria na watafikishwa mbele ya sheria. Moto katika meli hiyo umezimwa na tayari imepelekwa katika Bandari ya Sicilia.
|
Moshi mkubwa ukitoka katika meli hiyo baada ya wahusika kujitosa majini. |
|
MV Gold Star ikipelekwa katika Bandari ya Sicilia. |
No comments:
Post a Comment