Monday, April 1, 2013

PICHA MBALIMBALI ZA AJALI YA KUFUNIKWA NA KIFUSI JIJI ARUSHA


ajali (66)Mwili wa dereva wa lori moja kubwa lenye ujazo wa tani 18 ukiwa umeopolewa na askari jeshi, tayari kupelekwa mochwari ya Hospitali ya Mt Meru. Dereva huyu ametambulika kwa jina moja tu la Alex amefikwa na mauti akiwa  ndani ya gari hilo wakati vijana wengine wakiendelea kupakia moram  asubuhi ya leo

ajali (55)Mbunge wa Arusha Mjini, Mh Godbless Lema akiwasili eneo la ajali mapema asubuhi.
ajali (44)Baadhi ya wananchi waliojitokeza kushuhudia ajali hiyo mbaya wakishangaa zoezi la uokoaji na wengine wakisubiri kutambua ndugu zao, jambo ambalo  halikupata nafasi.
ajali (65)Mwananchi huyu aliishiwa nguvu baada ya kushuhudia mwili wa rafiki yake ukiopolewa kutoka kwenye kifusi
ajali (49)Hali ilivyo machimboni hapo
ajali (64)Kina mama wakilia kwa uchungu wakihofia kuondokewa na wapendwa wao
ajali (21)Vikosi vya Jeshi la Wananchi na Polisi vikiwa kazini
ajali (35)Sehemu ndogo ya Fuso ikionekana huku gari nyingine ikiwa haionekani kabisa.
________________________________________________________________________________

Inakadiliwa watu zaidi ya watu 18 wamepoteza maisha kufuatia  kufukiwa na gema la mchanga/moram wakati wakichimba na kupakia kwenye  malori eneo la Moshono jijini Arusha.
Ajali hiyo mbaya imetokea katika machimbo ya moram nje kidogo ya jiji eneo jirani na Moshono-Kiserian ambapo vijana hao  wanaokadiriwa kufikia idadi hiyo walikuwa wakipakia moram kwenye magari mawili, moja ni Fuso na lingine kubwa zaidi (tani 18) na yote mawili yamefukiwa kabisa na kifusi. 
Shuhuda mmoja wa ajali ambae pia ni  mchimbaji ameieleza Blog hii kwamba kwa kawaida gari ndogo kama Fuso  hupakiwa na watu 7, na hiyo kubwa huwa na watu 12 bila kuhesabu dereva na utingo. 
Miongoni wa waliofikwa na mauti ni pamoja na madereva wa magari hayo. Katika eneo la ajali hali ni ya simanzi na vilio toka kwa kina mama huku baadhi wa wababa na marafiki na ndugu wa jamaa waliofukiwa wakishindwa kujizuia na kuangua kilio. 
 
Meya wa  Manispaa Mh Gaudence Lyimo pamoja na Mbunge wa Arusha Mjini Mh Godbless  Lema ni miongoni mwa viongozi wakubwa waliofika eneo la ajali kusaidiana na kikosi cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania kufanya uokozi. 
 
Wachina wakipeleka moja ya mashine zao (Excavator) kuongeza nguvu katika kusaidia kufukua miili ya watu hao iliyonaswa na kifusi hicho.

Chanzo:
Picha/habari  
ARUSHA255 BLOG

No comments:

Post a Comment