Monday, April 1, 2013

WALIOFARIKI WAFIKIA 34 MTAA WA INDIRA GANDHI DAR


Idadi ya waliokufa kutokana na kuporomoka kwa jengo jijini Dar es Salaam, Tanzania, imefikia 34 asubuhi ya leo, kwa mujibu wa taarifa ya serikali.

http://vml1.s3.amazonaws.com/wp-content/uploads/2013/03/Tanzania.jpgBaada ya siku tatu za kuwatafuta manusura, inaripotiwa kuwa wafanyakazi wa huduma ya uokozi hawana tena matumaini ya kuwapata watu wengine walio hai. Jengo hilo la ghorofa 16 lililokuwa likijengwa katikati ya mji huo mkubwa kabisa nchini Tanzania liliporomoka siku ya Ijumaa, ambapo ni watu 17 tu waliopatikana wakiwa hai siku hiyo. Wengi wa waliokufa walikuwa vibarua na wapita njia. Wamo pia watoto waliokuwa wakicheza mpira karibu na jengo hilo. Mashahidi wanasema kwamba kuna vibarua wengi ambao hadi sasa hawajaonekana. Katika miaka ya karibuni, kuporomoka kwa majengo kumekuwa jambo la kawaida katika nchi za Afrika ya Mashariki, ambako wamiliki wa majengo hukwepa kanuni za ujenzi kwa lengo la kupunguza gharama.

No comments:

Post a Comment