Sunday, March 31, 2013

PAPA FRANCIS NA KADHIA YA SYRIA NA PENISULA YA KOREA


Papa Francis ameomba kufikiwa kwa ufumbuzi wa kisiasa nchini Syria na usuluhishi katika rasi ya Korea katika ujumbe wake wa kwanza wa Jumapili ya Pasaka mbele ya umati uliofurika katika uwanja wa Mtakatifu Petro. 

 http://news.bbcimg.co.uk/media/images/66684000/jpg/_66684489_francgetty.jpg
Papa huyo wa kwanza kutoka Amerika Kusini pia amesihi kuachiliwa kwa mateka wanaoshikiliwa na wanamgambo nchini Nigeria na kulaani usafirishaji haramu wa binaadamu kuwa ni aina ya utumwa wa hali ya juu katika karne hii ya 21. Papa ametowa baraka zake za kwanza za "Urbi et Orbi" kwa kuibariki Roma na dunia kwa jumla akiwa katika roshani ya Kanisa la Mtakatifu Petro ambapo alijitokeza mara ya kwanza kufuatia kuchaguliwa kwake kuwa papa mwezi huu.

No comments:

Post a Comment