Wanajeshi watano wa Afrika Kusini wameuawa wakati helikopta yao ilipoanguka katika doria ya operesheni ya kupiga vita ujangili.
Kwa mujibu wa taarifa ya kijeshi ajali hiyo ilitokea jana jioni katika Mbuga ya Taifa ya Kruger na uchunguzi tayari umeanza kubaini chanzo cha ajali hiyo. Afrika Kusini iko katika harakati za kukomesha uwindaji haramu wa vifaru ambapo pembe zao huuzwa kwa thamani kubwa barani Asia. Idadi ya vifaru waliouwawa nchini Afrika Kusini kuanzia mwaka huu imefikia 188 wakiwemo vifaru 135 kutoka Mbuga ya Kruger.
No comments:
Post a Comment