Tuesday, April 16, 2013

LAIZER AWATAKA WAFUGAJI WA KIMASAI KUPUNGUZA MIFUGO KWA KUUZA

Mbunge wa Jimbo la Longido Michael Lekule Laizer kwa titketi ya Chama cha Mapinduzi amewataka wafugaji wa kimasai katika Jimbo lake kupunguza mifugo hiyo kwa kuiuza ili kuongeza mapato yatokanayo na mifugo yao.

Katika mahojiano mapema leo asubuhi Mheshimiwa Lekule Laizer amesema endapo wafugaji wa kimasai watatambua kuwa mifugo waliyonayo ni rasimali tosha ya wao kukua kiuchumi basi itasaidia jimbo lake kuwa katika hali nzuri.

Laizer amesema kwa muda mrefu sasa kauli mbiu ya kupunguza mifugo imeonekana kutozaa matunda kutokana na mila na desturi za kimasai kutotaka kupunguza mifugo hiyo.

Pia ameongeza kusema kwa sasa kuna mabadiliko ya tabia nchi ambapo yamefanya hata mifugo kutoweza kufugika kwani hata katika jimbo lale kulitokea maafa ya ng’ombe kufa kutokana na misimu mitatu ya mvua kutonyesha katika ardhi yao.

Laizer amesema endapo watauza mifugo hiyo watatakiwa kuweka fedha zao benki kwa ajili ya matumizi mbalimbali ikwemo kujenga nyumba, kusomesha watoto.

Aidha Mbunge huyo amesema tangu mwaka 1995 alipoingia madaraka kulisimamia jimbo hilo amewatendea wananchi mahitaji muhimu huku akitajihidi kupitia serikali ya CCM iliyopo madaraka kukamilisha ahadi zake kwa wananchi.

No comments:

Post a Comment