Usaili wa waombaji uteuzi kwenye uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) na Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board) unaendelea na
unatarajia kukamilika leo (Septemba 1 mwaka huu).
Kamati ya Uchaguzi ya TFF chini ya Mwenyekiti wake Hamidu Mbwezeleni
ilianza usaili juzi (Agosti 30 mwaka huu) ambapo matokeo ya usaili
yanatarajiwa kutangazwa keshokutwa (Septemba 3 mwaka huu).
Kati ya Septemba 4 na 6 mwaka huu, Kamati ya Uchaguzi kupitia
Sekretarieti ya TFF itawasilisha kwenye Kamati ya Maadili ya TFF
mashauri yote ya maadili ili kujadiliwa na kutolewa uamuzi na kamati
hiyo.
Vilevile kati ya Septemba 4 na 6 mwaka huu ni kipindi cha kukata
rufani kwenye Kamati ya Rufani ya Uchaguzi kwa masuala yasiyo ya
maadili. Kwa watakaokata rufani wanatakiwa kuambatanisha na ada ya
rufani kwa Katibu Mkuu wa TFF kabla ya saa 10 kamili jioni ya Septemba 6
mwaka huu.
KIUNGO WA SIMBA AONGEZWA TAIFA STARS
Kiungo wa Simba, Jonas Mkude ameitwa kwenye kikosi cha Taifa Stars kinachojiandaa kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Gambia itakayochezwa Septemba 7 mwaka huu jijini Banjul.
Kiungo wa Simba, Jonas Mkude ameitwa kwenye kikosi cha Taifa Stars kinachojiandaa kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Gambia itakayochezwa Septemba 7 mwaka huu jijini Banjul.
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen amemuongeza mchezaji huyo ili
kuimarisha sehemu ya kiungo. Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro
Premium Lager imeingia kambini tangu Agosti 29 mwaka huu kwenye hoteli
ya Accomondia jijini Dar es Salaam.
Timu hiyo imefanya mazoezi leo asubuhi kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya
Karume wakati kesho Jumatatu (Septemba 2 mwaka huu) saa 10 jioni
itafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
WATATU WAOMBEWA ITC UJERUMANI
Chama cha Mpira wa Miguu cha Ujerumani (DBU) kimetuma maombi ya Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa wachezaji wawili wa Tanzania ili wajiunge na klabu mbili tofauti za nchini humo.
Chama cha Mpira wa Miguu cha Ujerumani (DBU) kimetuma maombi ya Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa wachezaji wawili wa Tanzania ili wajiunge na klabu mbili tofauti za nchini humo.
Maombi hayo yaliyotumwa kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) ni kwa ajili ya wachezaji Henry Claud Egito aliyezaliwa Desemba
31, 1984 jijini Dar es Salaam, na Dominic Johnson aliyezaliwa Agosti 14,
1991 jijini Tanga.
Wachezaji hao wanaombewa ITC kama wachezaji wa ridhaa. Egito
anaombewa hati hiyo ili ajiunge na klabu ya FSV Lokomotive Dresden
wakati Johnson anatakiwa na klabu na TSV 1967 Schwabbruck.
No comments:
Post a Comment