Siyo kundi la Sungusungu, Polisi Jamii au askari wa
makundi ya kiharakati au kisiasa unaoweza kufahamu. Hakuna ofisi wala
vikao wanavyokaa kusikiliza mashtaka kabla ya uamuzi, mbaya zaidi hakuna
anayejitambulisha kama mfuasi wa baraza hilo, lakini linatoa hukumu na
kutekeleza mauaji ya kutisha.
Taarifa zinaonyesha kuwa kwa mwaka jana pekee, wastani wa watu watatu walikuwa wakiuawa kila wiki na kikundi hicho cha watu kinachofahamika kama Baraza la Kimila katika Mkoa wa Simiyu, wakiwamo wanawake na watoto.
Wanachama wa kikundi hicho maarufu Dagashida,
hufahamiana muda wa kupokezana
‘Mbiu’inaposikika kama ishara ya kuhudhuria tukio la utoaji wa hukumu.
‘Mbiu’inaposikika kama ishara ya kuhudhuria tukio la utoaji wa hukumu.
Unaweza kulinganisha na Kundi la Al-Shabaab, kwani
baraza hilo hufanya maasi na kusambaa msituni kwa muda wa siku
zisizopungua tano wakihofia kutiwa mbaroni na Jeshi la Polisi.
Baraza hilo ni mfano wa kamati ya ulinzi au mahakama inayojiendesha kwa kufuata miiko na kanuni zake katikati ya Serikali inayoendeshwa kwa utawala wa sharia, likidaiwa kutoka Kabila la Wasukuma na jamii ya Kinyantuzu waliopo Mkoa wa Simiyu.
Mmoja wa maofisa wa ngazi za juu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu aliyeomba kutotaja jina lake gazetini kwa sababu za siyo msemaji wa polisi alithibitisha kutokea kwa mauaji hayo ya kikatili akishauri atafutwe mhusika ili atoe ufafanuzi kuhusu matukio hayo.
No comments:
Post a Comment