Wednesday, September 4, 2013

POMBE SI CHAI

 Vijana wawili wakazi wa manispaa ya Singida ambao hawakuweza kupatikana majina yao mara moja, wakiwa wamelala (saa nane mchana) kwa kile kilichodaiwa ni kutokana na kulewa kupitiliza. Wa kwanza kushoto inadaiwa awali alikuwa amelala juu ya bechi lakini alipozidiwa na usingizi, alidondoka chini na kuendelea kuuchapa usingizi. Katikati yao ni moja ya chupa ya pombe aina ya Banana waliyokuwa wanakunywa baada ya kumaliza viroba. Hivi karibuni kijana mmoja mkazi wa Kibaoni aliweza kuingiliwa kimwili kinyume na maumbile na rafiki yake,baada ya kulewa viroba kupindukia.

No comments:

Post a Comment