Sunday, May 5, 2013

BOMU LALIPUKA KANISA KATOLIKI PAROKIA OLASITI



http://arushacity.com/wp-content/themes/directorypress/thumbs//Arusha-Map-2012-Transparent-300x291.png
DURU za Habari kutoka Jijini Arusha hii leo zinasema mlipuko mkubwa umetokea katika Kanisa Katoliki Parokia ya  Olasiti  Jijini humo.

Taarifa zaidi zinasema watu kadhaa huenda wamejeruhiwa. Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuna watu walikuja na gari eneo la Kanisa hilo wakarusha kitu huku wengine wakidai kuwa kitu hicho kililipuka kutoka katika kifusi cha udongo uliomwagwa wa moramu.

Inasemekana kulikuwa na ugeni kutoka Vatican ambao ulikuja kufanya changizo kwa ajili ya ujenzi wa kigango mahali hapo.

Waliokuwemo ndani ya Kanisa hilo mapema leo asubuhi wanasema ni wakati Baba Askofu alipokuwa akibariki maji na kuweka chumvi (tendo la kubariki) ndipo mlipuko ulipotokea.

Inasemekana watu zaidi ya 20 wamefariki dunia licha ya taarifa hizo kutothibitishwa na Polisi.

Jeshi la Polisi halijatoa taarifa yake kuhusu tukio hilo.

HABARI ZAIDI HAPO BAADAYE….
.

No comments:

Post a Comment