Wito umetolewa kwa viongozi wa Halmashauri za Mkoani Kilimanjaro kufuatilia takwimu za miti iliyopandwa na kutunzwa ili kuifanya kampeni ya Upandaji miti katika maeneo mbalimbali mkoani hapa kuwa endelevu.
Akizungumza na Waandishi Habari ofisi kwake leo Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama amesema kumekuwa na udanganyifu mkubwa katika kampeni ya upandaji miti mkoani humo kwani kila mwaka kumekuwa na idadi zisizo za kweli katika upandaji wa miti.
Gama amesema kwa akili ya kawaida ni kwamba tangu mwaka 2000 ilipoanzishwa kampeni ya upandaji miti nchini nzima hadi sasa mkoa wa Kilimanjaro usingekuwa unalalamika kuongezeka kwa joto kupita hata maeneo yenye joto.
Mkuu huyo wa 22 kukalia kiti hicho mkoani Kilimanjaro amesema haitakuwa busara hata kidogo kupoteza muda na rasilimali kwa kupanda miti bila kufuatilia maendeleo ya ukuaji na utunzwaji wake.
Aidha Gama amesema serikali haitamuonea haya kumchukulia hatua za kisheria mtu yeyote atakayekiuka sheria zinazolinda mazao ya misitu na miti kinyume cha sheria.
Gama amehitimisha kwa kuwataka wananchi kujiepusha na uchomaji wa moto kichaa katika misitu kwani itasaidia kulinda uhai wa viumbe hai akiwemo binadamu.
No comments:
Post a Comment