Mwandishi mashuhuri wa vitabu nchini Nigeria Chinua Achebe, ambae alikuwa anatajwa kuwa ndie babu wa fasihi ya kisasa barani Afrika, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 82.
Msemaji wa kampuni ya Penguin ya mjini London inayochapisha vitabu vya Achebe alitangaza kifo chake kupitia barua pepe aliyoituma katika mashirika ya habari. Vyombo vya habari nchini Nigeria viliripoti kuwa Achebe alifariki katika hospitali mjini Boston, Massachusetts Marekani. Achebe alifahamika zaidi kutokana na kitabu chake cha hadithi cha 'Things Fall Apart' cha mwaka 1958, ambamo alizungumzia kisa cha msuguano baina ya watawala wa kikoloni wa Uingereza na utamaduni wa watu wa kabila la Igbo, katika eneo alikozaliwa kusini-mashariki mwa Nigeria.
No comments:
Post a Comment