Aidha mmiliki wa mbuzi huyo wakati akiongea na waandishi wa habari Clementina Masay alisema kuwamtuhumiwa huyo ambaye amekuwa akiwabaka mbuzi na kuwaingilia kwa nguvu amemsababishia hasara baada ya mimba ya mbuzi wake jike kuharibika.
Ameongeza kuwa Serikali inatakiwa imchukulie hatua kali mtuhumiwa huyo kwani baada ya kufikishwa Mahakamani na kufunguliwa kesi alipata dhamana lakini hadi hivi sasa ametorokea sehemu isiyofahamika.
Ameendelea kusema kuwa mtuhumiwa huyo,Daniel Marcel mwenye umri wa miaka 22 alifunguliwa kesi namba 29/2013 kwa kosa la kuiingilia mifugo,kinyume na kifungu cha 325 kanuni ya adhabu sura ya 16 na alipopata dhamana akatoroka.
Kesi hiyo ipo mbele ya Hakimu Julius Dagharo wa Mahakama ya Mwanzo Bashnet,ambaye ndiye aliyemsomea shtaka na Ofisa Mtendaji wa kijiji hicho Omari Mwanditi alikiri mshtakiwa huyo kutoroka baada ya kupatiwa dhamana.
Pia jamii ya wafugaji wa kiiraq wa eneo hilo wamesikitishwa na kitendo cha mifugo yao kuingiliwa mara kwa mara kwa kunajisiwa na walidai kuwa watamsaka mtuhumiwa huyo hadi wamkamate kwani kitendo hicho kimewasikitisha.
Aidha wamesema matukio ya mtuhumiwa huyo kuwaingilia mifugo yamekuwa yakitokea mara kwa mara na pindi anapoulizwa anadai kuwa anaiingilia mifugo kwa kuogopa kupata maambukizi ya virusi vya ukimwi.
No comments:
Post a Comment