Sunday, March 31, 2013

15 WAFA KATIKA MAPAMBANO NA BOKO HARAM

Wanajeshi leo wameyavamia maficho ya washukiwa wa kundi la itikadi kali za Kiislamu Boko Haram katika mji mkubwa wa kaskazini mwa Nigeria Kano, na kuchochea vurugu ambazo zimesababisha vifo vya watu 15.
 
http://www.csmonitor.com/var/ezflow_site/storage/images/media/content/2012/0321-boko/12077807-1-eng-US/0321-boko_full_600.jpgJeshi limedai kuwa waliouawa walikuwa ni pamoja na wanamgambo 14 wa Kiislamu na mwanajeshi mmoja, wakati likidai kuwa wapiganaji hao walikuwa wakipanga kufanya shambulizi la siku kuu ya Pasaka mjini humo. Wakaazi wamesema wamesikia milio ya risasi wakatai majeshi yakipambana na wapiganaji. Jeshi limedai kunasa silaha, ikiwa ni pamoja na gari lililokuwa na miripuko tayari kufanya shambulio.

No comments:

Post a Comment