Wahindu katika mto Ganges |
Mamilioni ya waumini wa madhehebu ya Hindu nchini India wamejitosa katika mto wao mtakatifu, Ganges, kitendo ambacho wanaamini kinawaosha dhambi zote.
Siku ya leo inachukuliwa kama siku yenye heri kubwa zaidi katika maadhimisho ya siku 55 yajulikanayo kama Kumbh Mela, ambacho umuhimu wake unatokana na masuala ya kinajimu. Afisa mkuu wa maadhimisho hayo Mani Prasad Mishra amesema kwamba tayari watu milioni tatu wamekwishaingia ndani ya mto Ganges kuanzia asubuhi, na kwamba wanategemea kuwa ifikapo jioni watu milioni kumi na moja watakuwa wamejiosha na maji ya mto huo yenye baridi kali. Wakereketwa wa dini ya Hindu wanaamini kwamba kuoga ndani ya mto Ganges kunaondoa dhambi zao, na kuwaepusha na mzunguko wa kifo na kuzaliwa kwa mara ya pili.
No comments:
Post a Comment