Ziara ya wanamuziki waliofanya vizuri mwaka 2012 maarufu kama
Kilimanjaro Music Tour 2013 iliyopewa kaulimbiu ya Kikwetu kwetu
imefanyika mkoani Kigoma na kuvunja rekodi ya mahudhurio katika uwanja
wa Lake Tanganyika baada ya maelfu ya wakazi wa mji wa Kigoma na maeneo
ya jirani kufurika kwa wingi kuwashuhudia wasanii wakali 12 waliopanda
jukwaani. Kivutio kikubwa katika tamasha hilo ilikuwa ni wanamuziki
wanne wanaounda kundi la Kigoma All Stars, Diamond, Mwasiti, Linex na
Recho kupanda mwishoni na kuimba wimbo wao maarufu wa Leka Dutigite na
kupata shangwe kubwa toka kwa mashabiki. Hizi ni baadhi ya picha za
matukio yaliyotokea.
No comments:
Post a Comment